TAASISI
ya Transparency International kupitia Bribe-Payers Index ilieleza kwamba,
Mobutu Seseko wa ‘Zaire’, Mohammed Suharto wa Indonesia na Ferdinand Marcos wa
Ufilipino kwa pamoja walifisidi nchi zao jumla ya Dola 50 bilioni, kiasi
ambacho kwa wakati huo kilikuwa sawa na bajeti nzima ya mwaka ya misaada kutoka
nchi wahisani.
Ripoti ya TI iliyoonyesha orodha ya wanasiasa mafisadi zaidi
wa miongo miwili iliyopita inaonyesha kwamba anayeongoza ni dikteta wa
Indonesia, Mohammed Suharto, lakini ripoti hiyo ikasema kwamba hakuna nchi
ambayo iko salama kwa rushwa na ufisadi, huku ikibainisha ufadhili wa kisiasa
nchini Ugiriki, uhusiano wa karibu kati ya makampuni kadhaa na utawala wa
familia ya Bush na utawala usio wa upinzani wa aliyekuwa waziri mkuu wa Italia,
Silvio Berlusconi.
Lakini ufisadi mkubwa zaidi umetokea katika nchi
zinazoendelea, ambako viongozi wamekomba rasilimali za mataifa yao na
kujilimbikizia mali.
Suharto alikomba takriban Dola 35 bilioni katika kipindi cha
utawala wake wa miongo mitatu kabla ya kufukuzwa wakati ambapo Mobutu yeye
alichota nusu ya Dola 12 bilioni za misaada ambazo zilitolewa na Shirika la
Fedha Duniani (IMF) kwa kipindi chote cha utawala wake na kuifanya nchi hiyo
ibaki na madeni makubwa hadi sasa.
Ndiyo
maana Ijumaa ya Mei 16, 1997 mara tu baada Laurent Desire Kabila kuipindua
serikali ya mwanahabari Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu
Wa Za Banga nchini Zaire, alitangaza kutaifisha mali zote za dikteta huyo
aliyeitawala kwa mkono wa chuma nchi hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa
miaka 32.
Siku
moja baadaye, yaani Jumamosi Mei 17, 1997 serikali ya Uswisi nayo ikatangaza
kuzuia mali za Mobutu kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kupokea maelekezo
kutoka kwa utawala mpya wa Kabila, ambaye wakati huo alikuwa ameweka makao yake
makuu jijini Lubumbashi.
Mali
zilizozuiliwa kufuatia uamuzi wa serikali ya Uswisi ni pamoja na hekalu lake
lenye vyumba 300 lililokuwa eneo la Savigny pembezoni mwa ziwa huko Lausanne,
ambalo kwa wakati huo thamani yake ilikuwa yapata Dola 5 milioni. Hili lilikuwa
miongoni mwa vitegauchumi vyake vingi tu barani Ulaya ambako ilielezwa kwamba
vyote kwa pamoja vilikuwa na thamani ya takriban Dola 37 milioni kwa wakati
huo.
Ingawa
kulikuwa na taarifa kwamba Mobutu, ambaye jina lake la ubatizo aliitwa Joseph-Desiré Mobutu, alikuwa ameficha karibu Dola 4 bilioni, lakini
serikali ya Uswisi ilichunguza katika benki zote 400 nchini humo na haikuona fedha zozote zilizowekwa kwa jina lake
au jina la wanafamilia wake.
Mobutu, ambaye alithubutu kulipa Dola 10 milioni kwa
mabondia Muhammad Ali na George Foreman (Dola 5 milioni kila mmoja) ili
wakapigane jijini Kinshasa Oktoba 30, 1974, hakuona shida yoyote kutumia fedha
hata kwenda kufanya ‘shopping’ Ulaya na ndiye rais pekee Afrika kutumia midege
mikubwa na ghali zaidi duniani, Concorde.
Mwaka
1989, Mobutu alikodi ndege ya Concorde yenye namba za usajili F-BTSD kutoka
Shirika la Ndege la Ufaransa (Air France) kwa ajili ya safari ya Juni 26– Julai
5 kwenda tu kutoa hotuba kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York,
Marekani, Julai 16 akakodi ndege hiyo kwenda Paris, Ufaransa kuhudhuria sherehe
za nchi hiyo baada ya kualikwa na Rais François Mitterrand, Septemba 19 akakodi
dege hilo kutoka Paris hadi mjini Gbadolite, Zaire na safari nyingine ya moja
kwa moja kutoka Gbadolite hadi jijini Marseille akiwa na kwaya ya vijana wa
Zaire.
Kwa
kutumia fedha za Wazaire, aliamua kujenga uwanja maalum mjini Gbadolite,
kaskazini mwa nchi hiyo ambako ndiko alikotokea, ili kuliwezesha dege la
Concorde litue na kuruka. Uwanja huo
uliokuwa kwenye kilele cha meta 460 kutoka usawa wa bahari, njia yake ya
kurukia ilikuwa na urefu wa meta 3,200 (kilometa 3.2) na upana wa meta 60.
Hata hivyo, ukiangalia katika orodha hiyo ya Transparency
International, majina yaliyomo ni ya viongozi ambao walikuwa wakilindwa na
kukingiwa kifua na Mataifa ya Magharibi ambayo yalifumba macho kutokana na
vitendo vilivyokuwa vikifanywa na watawala hao kama namna ya mabadilishano
wakati wa Vita Baridi.
Suharto, ambaye alifahamika kwamba ni mpinzani wa ujamaa
barani Asia, alikwiba takriban Dola 35 bilioni kutoka kwenye nchi hiyo wakati
wa utawala wake wa kidikteta kwa miongo mitatu, kabla hajang’olewa mwaka 1998
katika vurugu kubwa zilizoibuka kufuatia mdororo wa uchumi barani Asia.
Alishtakiwa kwa kukomba Dola 500 milioni kutoka serikalini
kupitia taasisi mbalimbali zilizoongozwa na familia yake, lakini majaji
wakasema alikuwa mgonjwa hivyo hakustahili kusimama mahakamani.
Marcos, ambaye mkewe alikuwa na jozi 3,000 za viatu alikuwa
msamiati maarufu kutokana na rushwa aliyoitenda wakati wa utawala wake, lakini
alikuwa kipenzi cha Marekani na hawakuwahi kumnyoonyeshea kidole.
Jitihasa za kuzisaka Dola 10 bilioni alizokwiba wakati wa
utawala wake wa miaka 20 hazikuweza kuzaa matunda na zilivurugwa kutokana na
sheria kali za kibenki nchini Uswisi. Mnamo Agosti 2003, miaka 14 baada ya kifo
chake, mahakama za Uswisi hatimaye ziliamuru Dola 657 milioni za dikteta huyo zilizofichwa
nchini humo zirudishwe kwa serikali ya Ufilipino.
Mobutu alitumia hil na vitisho kwamba angeweza kuivamia
serikali ya Angola iliyokuwa na mrengo wa Marxist ili kuwanyamazisha watawala
wa mataifa ya magharibi wasimnyooshee kidole kuhusu namna alivyokuwa anaiba
rasilimali za taifa lake ambalo linaongoza kwa kuwa na madini mengi barani
Afrika. Marekani iliishawishi IMF
iendelee kuipatia Zaire mikopo, licha ya mashaka makubwa waliyokuwa nayo
maofisa wa IMF dhidi ya utawala wa dikteta Mobutu.
Mpaka anapinduliwa mwaka 1997, Mobutu alikuwa ameiba karibu
nusu ya Dola 12 bilioni za misaada ambazo Zaire ilipata kutoka IMF wakati wa
utawala wake wa miaka 32, akiiacha nchi yake ikiwa na mzigo mkubwa wa madeni.
Ripoti ya Global Financial Integrity (GFI)
ya mwaka 2008 ilionyesha kwamba kumekuwa na ongezeko la kiasi cha fedha
kinachotoroshwa katika nchi mbalimbali duniani kutoka Dola za Marekani 1.06
trilioni za mwaka 2006 hadi kukaribia Dola 1.26 trilioni za mwaka 2008.
Katika kiasi hicho cha fedha, wastani wa
Dola 725 bilioni hadi 810 bilioni zilitoroshwa kwa mwaka tangu mwaka 2000 hadi
2008 kutoka katika nchi zinazoendelea.
Ripoti hiyo inaonyesha pia kwamba,
Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, zinaongoza kwa asilimia 24.3, nchi
zinazoendelea za Ulaya asilimia 23.1, Afrika asilimia 21.9 na Asia asilimia
7.85.
Katika ripoti hiyo, nchi 10 zinazoongoza duniani
kwa kuwa na kiwango kikubwa cha fedha kilichotoroshwa kati ya mwaka huo 2000
hadi 2008 na kiasi katika mabano ni China (Dola 2.18trilioni), Russia (Dola
427bilioni), Mexico (Dola 416 bilioni), Saudi Arabia (Dola 302bilioni),
Malaysia (Dola 291bilioni), Umoja wa Falme za Kiarabu (Emirates, Dola 276
bilioni), Kuwait (Dola 242bilioni), Venezuela (Dola 157bilioni), Qatar (Dola
138bilioni) na Nigeria (Dola 130bilioni).
Ifuatayo ndiyo orodha ya marais ‘wezi na mafisadi’ zaidi
duniani katika kipindi cha miongo 20 iliyopita;
Mohammed
Suharto
Taifa - Indonesia,
1967-98
Kiasi - Dola15bn hadi 35bn
Kiasi - Dola15bn hadi 35bn
Ferdinand
Marcos
Taifa – Ufilipino, 1972-86
Kiasi - Dola 5bn hadi 10bn
Kiasi - Dola 5bn hadi 10bn
Mobutu
Sese Seko
Taifa - Zaire, 1965-97
Kiasi – Dola 5bn
Kiasi – Dola 5bn
Sani
Abacha
Taifa - Nigeria, 1993-98
Kiasi – Dola 2bn hadi 5bn
Kiasi – Dola 2bn hadi 5bn
Slobodan
Milosevic
Taifa - Serbia, 1972-86
Kiasi - Dola 1bn
Kiasi - Dola 1bn
Jean-Claude
Duvalier
Taifa - Haiti, 1971-86
Kiasi – Dola 300m hadi 800m
Kiasi – Dola 300m hadi 800m
Alberto
Fujimori
Taifa - Peru, 1990-2000
Kiasi - Dola 600m
Kiasi - Dola 600m
Pavlo
Lazarenko
Taifa - Ukraine 1996-97
Kiasi – Dola 114m hadi 200m
Kiasi – Dola 114m hadi 200m
Arnoldo
Alemán
Taifa - Nicaragua, 1997-2002
Kiasi – Dola 100m
Kiasi – Dola 100m
Joseph
Estrada
Taifa - Ufilipino, 1998-2001
Kiasi – Dola 78m hadi 80m
Kiasi – Dola 78m hadi 80m
Hii kwa mujibu wa maendeleo vijijini










Post a Comment