Kuna usemi wa Kiswahili usemao, “ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo”.
Usemi
huo unaweza kusawili tukio lililozuka juzi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi mkoani Dodoma baada ya mzazi wa mtoto anayedaiwa kupewa mimba na
mwalimu wake, kuangua kilio nje ya Mahakama.
Mzazi
huyo, Ayubu Mdachi aliangua kilio hicho kutokana na mwalimu Adeodatus
Rutajama (30) anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi wake kuachiwa huru.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alimuachia huru mwalimu huyo
baada ya kukosekana kwa ushahidi wa moja kwa moja kumtia hatiani
Rutajama kuhusika na tukio la kumpa mimba mwanafunzi wake wa miaka 15.

Post a Comment