Mtandao utabanwa DRC kwanzia Jumapili hii
Kampuni za mitandao
katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeamrishwa kufunga mitandao
ya kijamii kwanzia Jumapili hii. Hii ni kwa mujibu wa shirika la habari
AFP.
Mmoja wa maafisa wa kampuni ya mtandao ameambia AFP kamba
wamepokea amri hiyo kutoka kwa serikali kubana mtandao wote. Muhula wa
Rais Joseph Kabila chini ya katiba unatarajiwa kumalizika Jumatatu ya
wiki ijayo.
Wanaharakati wameanzisha kampeini kwenye Twitter
#ByeByeKabila, kama njiya ya kumshinikiza kiongozi huyo kuachia ngazi.
Chini ya katiba ya DRC Rais Kabila alistahili kumaliza muhula wake
Decemba mwaka huu na kufanyike uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo tume ya
uchaguzi ilisema haikuwa tayari kuanda uchaguzi. Mazungumzo ya kitaifa
ambayo yalisusiwa na vyama vikuu vya upinzani yalipendekeza uchaguzi
kuahirishwa hadi mwaka 2018, ambapo Kabila ataongoza kipindi cha mpito.
Licha
ya kwamba mahakama ya kuu imeridhia makubaliano hayo, hata hivyo
wapinzani wamesema lazima Kabila aondoke madarakani kwanza na kuundwe
utawala wa mpito bila yeye kuongoza.
Rais huyo ameahidi kwamba
hatagombea mwaka 2018, lakini wapinzani wamepinga hilo. Kumekua na
maandamano yaliokumbwa na ghasia na vifo kushinikiza Joseph Kabila
kuheshimu katiba ya nchi na kustaafu. Katiba haimkubalii kuwania Urais
tena baada ya kumaliza mihula miwili.
Post a Comment