
………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
IMEELEZWA
kuwepo kwa sakata la kutokea kwa migogoro ya ardhi kila kukicha katika
Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na
baadhi ya watendaji wa vijiji kuendekeza masuala ya rushwa ,ufisadi na
kuuza maneo kiholela hali ambayo inasababisha kuchochea vurugu na
mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii ya wakulima na wafugaji .
Hayo
yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa wakati wa
ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali
za kimaendeleo pamoja na kuona changamoto zinazowakabili wananachi
wake ili kuweza kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mchengerwa
alisema kwamba katika Jimbo lake la Rufiji kumekuwepo na baadhi ya
wenyeviti wa vijiji na watendaji kuwa na tamaa kwa kuamua kuuza hekari
moja ya ardhi kwa kiasi cha shilingi elfu tisa hali ambayo amedai hawezi
kuwavumilia na atakikisha anashirikiana na viongozi wa serikali kuvunja
mikataba yote kwa wawekezaji waliojipatia maeneo kinyume cha sheria.
“Jamani
wananchi wangu kwa hili suala mimi siwezi kukubaliana nalo hata kidogo
yani baadhi ya watendaji wa vijiji wanafanya mambo kinyume cha sheria na
taratibu kabisa, wanauza ardhi kwa bei ya shilingi elfu tisa, hapa hili
nitalivalia njuga na wawezezaji wote walionunua maeneo inabidi tukae
nao tena chini kuwekeana mikataba hii sio sahihi hata kidogo,”alisema
Mchengerwa.
Aidha
Mchengerwa katika hatua nyingine alisema kutokana na kuwepo na hali ya
sintofahamu kwa wananchi wa kata nzima ya Chumbi kuhusiana na suala
zima la baadhi ya watendaji wa kijiji hicho kutuhumiwa kuhusika
kujihusisha na uuzaji wa maeneo na kufanya ubadhilifu wa fedha
amewataka kutomkaribisha mwekezaji wa yoyote mpaka Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Injia Evarist Ndikilo atapokwenda kusikiliza kilo chao na
kulitatua sakata hilo la ardhi.
Pia
Mchengerwa alisema kuwa maeneo mengi yameuzwa bila ya kuzingatia
sheria na taratibu, hivyo katika eneo la kijiji cha Chumbi anatambua
kuna migogoro mingi ya ardhi hiyo katika kulitataua suala hilo
atahakikisha anashirikiana na viongozi wa ngazi ya Mkoa kwa lengo la
kuweza kurudisha ardhi ambayo imechukuliwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi Salumu Mtimbuko ambaye pia
ni Diwani wa kata ya Chumbi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika uuzaji
wa ardhi kiholela na ubadhilifu wa fedha na wananchi alisema kwamba kuna
baadhi ya wawekezaji wamenunua zaidi ya hekari 2900 wakati yeye bado
ajaingia maadarakani.
WANANCHI
wa kijiji cha Chumbi A,B,na C kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa
Pwani kwa sasa wanakabiiwa na sakata la kuwepo kwa migogoro mikubwa ya
ardhi inayosababishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kujiuzia maeneo
kiholela bila ya kuzingatai sheria na taratibu zilizowekwa hali
inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani.