0

 Mbwana Samatta ana urafki wa karibu na mchezaji mwenzake kutoka Nigeria anaitwa Wilfred Ndidi ambae ana umri wa miaka 19. Kwa habari ambazo zinaripotiwa sasa hivi ni kwamba mchezaji huyu anatarajiwa kusainiwa na Leicester City au Manchester united baada ya scounts wa timu hizi mbili kujiridhisha.

Lakini nafasi kubwa ni kwenda kujiunga na foxes ambao wana pengo la Ngolo Kante ambae anaisaidia vizuri Chelsea kwa sasa hivi. Leicester wamedhamilia kutoa pound milioni 15 ili kumsajili mchezaji huyu.

Imekua kawaida sana kwa club kubwa kuchukua wachezaji kutoka KRC Genk ambao wanasifika kwa kufanya good scouting na kuwakuza vizuri wachezaji. Benteke ni mmoja kati ya wachezaji waliopitia Genk na kupata mafanikio kwenye club kama Liverpool.

Post a Comment

 
Top