0
TIMU ya Hawili FC (U-14) imetawazwa kuwa mabingwa wapya  wa Ligi ya Jogoo leo desemba 27 baada ya timu ya Wakota fc kutofika uwanjani kucheza fainali na  kupewa pointi za mezani kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mbaya iliyopo kijiji cha Mbaya kata  ya Mbaya wilaya Liwale mkoani Lindi. 
 
Ligi ya Jogoo leo desemba 27 imemalizika rasmi mara baada ya kuanza kutimua vumbi Desemba 12 mwaka huu na kushirikisha jumla ya timu 4 ambazo ni mchweke fc, toto sinza fc, wakota, Hawili fc Timu ya Hawili fc.

Katika hatua ya fainali iliyokuwa ipigwe hii leo katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbaya Timu ya Wakota fc ilitarajiwa kuvaana na  Hawii ambao hadi muda wa mchezo unafika haikuweza kutokea uwanjani na kupelekea Hawili fc kuibuka mshindi kwa kuchukua pointi za mezani
 
Hadi tunaingia mitamboni sababu halisi za timu ya Wakota fc kutofika uwanjani bado hazijajulikana
 
 Kapteni wa timu ya Hawili fc, Shanibu mandandu amesema mashindano hayo yameweza kuongeza ushirikiano mkubwa kwa wachezaji na kuibua vipaji vilivyojifisha.

 Katika hatua nyengine Shanibu  amewaomba wadau wa soka hapa nchini kujitokeza kudhamini mashindano mengine yanayofanana na hayo kwa lengo la kuibua vipaji vilivyojificha katika kata ya Mbaya
 Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo seif Kimbwanda amesema kushindwa kufika timu ya Wakota fc ni pigo kubwa kwani alitegemea fainali kuona wachezaji wakionesha uwezo wao pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wa soka hapa nchini kujitokeza kudhamini mashindano mbali mbali ya Vijana pindi yanapofanyika 

Post a Comment

 
Top