Hatimae mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemaliza mgogoro wa maji
uliokuwa unahusiha vijiji 27 uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano ambapo
wananchi walikuwa wakigombea chanzo cha maji cha Nkoasenga kilichopo
katika kata ya Leguruki wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mgogoro kati ya wananchi hao umesababisha kusimama kwa huduma za maji kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili ambao ulifikia hatua ya wanannchi hao kuhujumu miundombinu ya maji kwa kukata mabomba yanayopeleka maji vijijini na kuwasababishia wananchi adha kubwa ya maji.
Wakizungumza katika mkutano wa wananchi ulioitishwa na mkuu wa mkoa na kuhusisha viongozi wa mkoa, wilaya pamoja na bodi ya maji ya MAKILENGA wananchi hao walimfikishia Gambo malalamiko yao ili waweze kupata huduma hiyo.
Mara baada ya kusikiliza kero za wananchi hao Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akatoa maagizo.
Kufuatia Maagizo hayo wananchi wa Kata ya Leguruki wamemaliza tofauti zao na kuhitimisha mgogoro huo ambao ulidumu kwa miaka mingi na kusababisha hasara licha ya mradi huo kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.

Post a Comment