Askari wa kikosi cha Suma JKT, Moses Mwita amefariki dunia baada ya kujipiga na risasi sehemu ya kifua.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio la askari kujiua
limetokea jana saa 4:15 asubuhi katika kituo cha mafuta cha BMC Mlimani
kilichopo mtaa wa Bugando ambapo askari huyo alijiua kwa kutumia silaha
aina ya Shortgurn.
Msangi
alisema taarifa za awali zilibaini kuwa askari huyo alionekana
akizungumza na simu kwa muda mrefu kana kwamba kulikuwa na tatizo
lililokuwa linamtatiza na baada ya muda alizunguka nyuma ya kituo na
kujipiga risasi kifuani hivyo kusababisha kifo chake.
Post a Comment