Kufuatia kasi ndogo ya usafirishaji wa zao la korosho kupitia bandari ya Mtwara , Wanunuzi wa zao la korosho katika mkoa wa Lindi wamesema uwezo mdogo wa bandari ya Mtwara kupokea kiasi kikubwa cha korosho na kwa muda muafaka kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi , kunachangia bei ya zao hilo kushuka,huku serikali ya mkoa ikipokea changamoto hizo na kuruhusu wanunuzi kusafirisha kwa njia magari.
Wakitoa maombi yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, baadhi ya
wanunuzi wa zao hilo wameiomba serikali kuifanyia maboresho Bandari ya
Mtwara na kusisitiza kuwa biashara ya korosho ina muda maalumu na
ifikapo January 2017 wanunuzi wote wanahamia nchi nyingine zilizoivisha
zao hilo.
Wakijadili hali hiyo baadhi ya wanunuzi akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa
Bodi ya Korosho Tanzania,Hassan Jarufu pamoja na wawakilishi wa wananchi
wa mkoa wa Lindi walibainisha hali inayokwamisha zao hilo kwa sasa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi katika
kukabiliana na hilo ameagiza wanunuzi kufuata taratibu za vibali toka
Bodi ya Korosho na Kuanza Usafirishaji.Channel ten
Post a Comment