0

 Wakulima wa zao la korosho wa vyama vya ushirika Ruangwa,Nachingwea na Liwale (RUNALI) akiwa kwenye mnada wa sita uliofanyika wilaya ya leo leo novemba 20 na kuazimia kukataa kuuza korosho zao kwa bei ya chini iliyotangwaza mnadani hapo. 

Wawakilishi wa wakulima 2 walioudhulia kwenye zoezi la kufungua sanduki la tena 
wakulima walioudhulia kwenye mnada wa sita uliofanyika leo novemba 20 wilayani Liwale

Meneja wa  RUNALI, Christopher Mwaya ikijuisha vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) vilivyopo katika wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale
Makamo mwenyekiti wa Runali,Bw. Hasani Mpako
 Mwakilishi wa wakulima akizungumza kwenye mnada wa leo novemba 20 ikiunga mkono kukataa kuuza korosho zao kwa bei ya chini
Mwakilishi wa wakulima akizungumza kwenye mnada wa leo novemba 20 ikiunga mkono kukataa kuuza korosho zao kwa bei ya chini
Mwakilishi wa wakulima akizungumza kwenye mnada wa leo novemba 20 ikiunga mkono kukataa kuuza korosho zao kwa bei ya chini
Viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya ushirika walioudhulia kwenye mnada wa korosho
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi (kushoto) na mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Kiwamba
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi,mhe. Hassan Masala
          mbunge wa jimbo la Liwale,mhe.Zuberi Kuchauka
Mkuu wa mkoa Lindi,Godfrey Zambi akizungumza kwenye mnada wa korosho na wakulima wilayani Liwale.


Mnada wa Sita wa korosho unaosimamiwa na kuratibiwa na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, umesitishwa kutokana na wakulima kutoridhika kuuza kwa bei ya chini na wakidai kuna hujuma imetokea.

 Meneja wa chama hicho, Christopher Mwaya, alithibitisha kusitishwa mnada huo leo novemba 20 na kusogezwa mbele, Meneja huyo ambae chama chake kinasimamia na kuratibu kazi za vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) vilivyopo katika wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale, alisema mnada huo hautafanyika kama ilivyotarajiwa na  utafanyika siku ya alhamisi novemba 24.

Hatua hiyo ilifikia baada ya kampuni za tenda za kununua korosho kupungua zaidi na kufikia kampuni 6 na kutaka kununua chini ya kiasi cha shilingi 3150 kwa maghala ya Liwale na Lindi farmers.

Makamo mwenyekiti wa Runali,bw. Hasani Mpako alisema katika mnada huo alidai kuwa kuna hujuma au uzembe wa bodi ya korosho ambazo zimefanyika na kuwataka wakulima kukataa kuuza korosho kwa bei ya chini.

Mpako alisema matangazo ya mnada huo hasa kuhusu kiasi cha korosho zilizotarajia kuuzwa hayakutolewa kwa wakati.

Hivyo kusababisha wanunuzi wengi kukosa taarifa na kusababisha  kujitokeza wafanyabiashara hao wachache ambao hata bei walizoomba kununulia zilikuwa za chini kuliko za minada mitano iliyopita.
 
"Watendaji wa RUNALI walifanyajitihada kubwa na walitimiza wajibu wao, walishapeleka taarifa mapema bodi ya korosho. Katalogi(orodha ya kiasi cha bidhaa ), hata hivyo katalogi ya bodi  ilipokelewa saa tano na mtandao ulikuwa unamaandishi yasioleweka," alisema Mpako.

Alisema iwapo matangazo yangetolewa mapema kungekuwa na uwezekano wa wanunuzi wengi kujitokeza. Hivyo kungekuwa na ushindani ambao ungesababisha kupandisha bei. 

Akiongeza kusema "Nijambo la kushangaza kusikia kampuni zilizojitokeza kwenye mnada huu ni sita wakati msimu huu kunakampuni 66 ziliomba kununua," alisema.

Mhasibu  wa chama cha msingi Mirindimo, Ahmad Makokola, alisema mfumo wa ununuzi ulipoanza  ulionesha ungekuwa na manufaa kwa wakulima. Hata hivyo kadiri siku zinavyokwenda, matumaini ya kunufaika yanapungua." Kwakuzingatia maelezo ya makamo mwenyekiti, mimi sipotayari kuuza korosho za chama changu kwenye mnada huu, nawashauri nawenzangu tusikubali kuuza.

Nae mwenyekiti wa chama cha msingi cha Mchangani, Maliki Maluchila alisema kutokana na kutoridhishwa na mchakato wa matangazo ya kuwapata wafanyabiashara na bei ndogo, yeye kama kiongozi wa wachama cha msingi ambacho ni mali ya wakulima, hakuwatayari kuuza korosho za wakulima hao katika mnada huo.

Mkulima Abeid Mtamajagi wa kijiji cha Liwale B, alisema hali hiyo inazidi kuwakatishatamaa wakulima na kuwaongezea maumivu. Kwamadai kwamba hata ambao korosho zao zilinunuliwa kwenye minada iliyopita hawajalipwa. 

Alisema hali hiyo itawafanya wauze korosho kwa walanguzi. Kutokana na maelezo ya wakulima hao walioudhulia kwenye mnada huo.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi,mhe. Hassan Masala pamoja na mbunge wa jimbo la Liwale,mhe.Zuberi Kuchauka kwa pamoja waliwaunga mkono wakulima. 

Nae mkuu wa mkoa Lindi,Godfrey Zambi aliwata viongozi wa Runali kurudia mnada huo wiki ijayo siku ya alhamisi novemba 24 na aliongeza kusema kuwa kama kulijitokeza na  dosari wazirekebishe na ofisi yake suala hilo watalifuatilia ili kubaini kama kuna njama za kodi ya korosho kupanga njama ya kushusha bei hiyo.

Katika mkutano huo Meneja wa Runali,Christopher Mwaya  wamehakikishiwa wakulima wa chama cha Runali kulipwa fedha zao siku ya jumatatu novemba 21 kwa wale waliuza mnada wa kwanza.


SILIZA MENEJA WA RUNALI AKITOE UFAFANUZI YA MALIPO,NA WABUNGE WA NACHINGWEA NA LIWALE WAKIWAUNGA WANANCHI WAO PIA NA MKUU WA MKOA AKIONGELEA SAKATA HILO.

Post a Comment

 
Top