Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi
KATIKA
hali inaoyoonesha kukosekana mahusiano mema baina ya wakulima na
wafugaji wa kata ya Somanga wilaya ya Kilwa. Baadhi ya wakulima na
wafugaji wakata hiyo walijitahidi kumshawishi kwa maneno na vitendo
mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi awaonee huruma. Huku kila upande
ukiutuhumu upande mwingine kuwa ni chanzo kitakacho sababisha uvunjifu
wa amani katika kata hiyo.
Hayo
yalitokea kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mkuu huyo wa mkoa,
uliofanyika katika kijiji cha Somanga, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wakulima
waliwatuhumu wafugaji kuwa ni chanzo cha kuvurugika mahusiano mema
kutokana na tabia zao za ubabe, ikiwamo kulisha mifugo kwa nguvu kwenye
mashamba yao.
Wakati
wa wafugaji waliwatuhumu wakulima kuwa wanawatisha wanapo kuwa
machungani na kuikatakata kwa mapanga mifugo yao bila sababu.
Baada
ya Zambi kutoa nafasi ya kuuliza maswali na kueleza kero zao baada ya
kumaliza hotuba yake iliyokuwa imezungumzia maagizo mbalimbali ya
serikali na mipango ya maendeleo ya mkoa huo. Ndipo wakulima na wafugaji
hao wakaweka wazi kuwa mahusiano baina yao sio mazuri na wanaishi kwa
uhasama mkubwa.
Hivyo
mkuu huyo wa mkoa aupatie uvumbuzi mgogoro huo. Hata hivyo wakulima na
wafugaji hao katika kumshawishi walikuwa wanasema kweli na wanahitaji
kuhurumiwa ndipo kila mmoja alitumia mbinu yake kumshawishi.
Aliyeanza
kuzungumza kwa upande wawakulima alikuwa, Upendo Ulaya ambae wakati
anazungumza alikuwa amepiga magoti na kunyanyua mikono juu mithili ya
mkosaji aliyekuwa anaomba radhi mbele ya mtu aliyemkosea.
Pendo
alisema wafugaji wamekuwa ni miongoni mwakero zinazohitaji kutatuliwa
na mkuu huyo wa mkoa, kwa madai kuwa tatizo hilo lina muda mrefu. Hata
hivyo halijapata suluhisho. Alisema wafugaji wanalisha mifugo yao kwenye
mashamba wanapowauliza wanajibiwa kuwa mifugo inathamani kuliko mazao
ya kilimo na hawaogopi chochote.
Huku akiwa amepiga magoti na kunyanyua mikono juu alisema:
"Baba
tuokoe wanao tunapigwa na wafugaji, mazao yetu yanaliwa na ng'ombe.
Tukilalamika kwa viongozi wetu tunawekwa ndani, hatuna kwa kwakwenda
kulalamika nakusikilizwa hali nimbaya baba," alisema Upendo.
Nae mfugaji Bangili Nganga Mbeho alisema wafugaji hasa vijana wanaochunga mifugo usalama wao upo mashakani.
Kwamadai
kwamba wanatishwa na mifugo yao inakatwa na mapanga inapokuwa
malishoni. Hata kama haijaingizwa kwenye mashamba. Mfugaji huyo huku
akitiririkwa na machozi alisema:
"Wafugaji
tunawindwa tunaishi kwa hofu, vijana wetu wakiwa machungani wanatishwa,
ng'ombe wetu wanakatwa mapanga. Sisi niwa Tanzania twende wapi mkuu wa
mkoa," alilalamika.
Mfugaji huyo alisema chanzo cha mgogoro ni wakulima kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mifugo nakulima mashamba. Hivyo maeneo yakufugia yamelimwa mashamba, na kusababisha eneo la kufugia kuwa dogo.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa, Zambi alisema ofisi yake itaunda tume haraka
ambayo jukumu lake litakuwa nikubaini chanzo halisi cha mgogoro huo na
kushauri njia bora zitakazo tumika kupata suluhisho la kudumu la mgogoro
huo.
Aliwataka
wakulima na wafugaji hao kuacha kuhasimiana, waheshimu mipaka
iliyowekwa kisheria na waishi kama ndugu. Alisema asingependa kuona
wananchi hao wanaishi kwa mfumo huo unaotishia amani na utulivu.
Huku akibainisha kuwa kila mmoja anawajibu wa kuheshimu kazi halali ya mwenzake.
"Kila
mmoja ameonesha kuvutia kwake, ni hali inayoonesha kuwa kuna mgogoro,
nitaunda kamati ambayo itawashirikisha wawakilishi wa wakulima na
wafugaji," alisema Zambi.
Mkuu
huyo alitoa ushauri kwa wakulima nawafugaji hao wajenge utamaduni kabla
ya kuingia kwenye migogoro, wakulima kilimo cha kisasa
iliwaweze kuzalisha mazao mengi kwenye maeneo madogo na wafugaji wafuge
kiasi cha mifugo kinachoweza kuhimili maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji.
Mgogoro
huo uliwahi kuingiliwa kati hivi karibuni na mkuu wa wilaya hiyo,
Christopher Ngubiagai kuagiza wafugaji waache tabia ya kwenda kufugia na
kulisha kwenye vijiji na maeneo yasiyotengwa kwa ufugaji na waondoke
kwenye maeneo na vijiji hivyo.
Pia
wakulima waliovamia na kuweka mashamba kwenye maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya ufugaji waondoke kwenye maeneo hayo. Agizo ambalo pia
limelalamikiwa na baadhi ya wakulima kwenye mkutano huo.
Post a Comment