Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 13
ya watoto huzaliwa wakiwa na uzito pungufu (Njiti) nchini Tanzania hali
ambayo huchangia asilimia 86 ya vifo vya watoto wachanga.
Takwimu hizo zimetolewa jana Jijini Dar
es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospital ya Taifa
Muhimbili Dkt. Julieth Magandi ikiwa leo Tanzania inaungana na mataifa
mengine zaidi ya 60 duniani kuadhimisha siku ya watoto njiti duniani
ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17.
Amesema katika kuhakikisha wanapunguza
vifo vya watoto njiti nchini serikali kwa kupitia Wizara ya Afya kwa
mara ya kwanza wameanza kutoa dawa ya kukomaza mapafu kwa watoto
waliozaliwa njiti na kuwezesha kufanikisha kupatikana kwa mashine kumi
za kupumulia watoto wachanga.
Amesema kutokana na uhaba wa upatikanaji
wa mashine za Oxygen, ni mashine nne pekee ndizo zinaweza kutumika kwa
mara moja hali ambayo inaleta shida kwa watoto wengine kukosa huduma
hiyo ikilinganishwa na idadi ya watoto wanaohitaji huduma hiyo na
jitihada zaidi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya kuwa na
kitengo cha watoto wachanga mahututi Neonatal ICU.
Amesema gharama za kununulia dawa za
kukomaza mapafu ni kubwa sana kwa Hospitali, idadai ya watoto ni kubwa
sana ukilinganisha na nafasi za iliyopo hivyo ni watoto wachache
wanaobahatika kupata huduma na uhaba wa vifaa tiba vya kutoa huduma kwa
watoto hao.
Post a Comment