0

Serikali ya Japan imetoa msaada wa dola 126,726 sawa na Sh 268 milioni  kwa Taasisi ya Benjamin Mkapa  kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Nkoma kilichomo Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Utiaji saini wa fedha hizo  umefanyika leo  ubalozi wa Japan jijini Dar es salaam baina ya Balozi Masaharu Yoshida wa Japan na mkurugenzi wa taasisi hiyo Dk. Ellen Senkoro

Balozi Masaharu amesema Japan imetoa msaada huo ili kuokoa maisha ya akina mama wajawazito ambao wamekuwa wakipoteza maisha wakati wa kujifungua.

Dk Senkoro amesema ujenzi wa chumba hicho cha upasuaji utaona maisha ya wajawazito na watoto ambao hulazimika kusafiri kwa zaidi ya kilomita 40 kutafuta huduma ya upasuaji.

Post a Comment

 
Top