Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama leo amewatunukia kamisheni
maafisa wanafunzi wa kijeshi 194 katika sherehe zilizofanyika katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam
Katika sherehe hizo Rais alikagua gwaride kabla ya kuwatunukia kamisheni maafisa hao na baadaye kushuhudia gwaride la kimyakimya lililooneshwa na askari kutoka kambi ya Abdalah Twalipo ya jijini Dar es Salaam na kisha bendi ya jeshi hilo kupita mbele ya amiri jeshi mkuu ikiwa ni sehemu ya burudani ya sherehe hizo.
Kamisheni hiyo ni ya 59 ya maafisa wanafunzi wa jeshi kutunikiwa baada ya mafunzo ya mwaka mmoja katika chuo kikuu cha maafisa wa kijeshi Monduli Mkoani Arusha na ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na maafisa waandamizi wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ.
Akitoa taarifa fupi ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paul Peter Masao amesema katika mafunzo hayo, jumla ya wanafunzi 221 ndiyo walioanza, lakini waliohitimu ni 194, huku wengine 27 wakishindwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali.
Pia amesema mmoja kati ya 194 waliotunukiwa kamisheni hizo leo, alipatia mafunzo yake nchini Uingereza ambapo kwa mujibu wa utaratibu, anapaswa kuungana na wenzake nchini kwa ajili ya zoezi hili mbele ya Amiri Jeshi Mkuu.
Hii ni mara ya kwanza kwa tukio hilo kufanyika nje ya chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Monduli, tangu chuo hicho kihamishiwe Monduli mkoani Arusha kutoka Jijini Dar es Salaam mwaka 1976.

Post a Comment