0

LEO Novemba 25, 2016 wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es SalaamRC Paul Makonda ambaye ameanzisha kampeni maalum ya #DAR_MPYA amekuwa akizunguka kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wananchi ili kufahamu na kutafua kero zinazowakabili.
, Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Wialaya ya Ubungo huku wakieleza kero zao mbalimbali kwa Mkuu wa mkoa huyo, ikiwemo kuvunjiwa nyumba zao na TANROADS kupisha barabara, huku wakidai kuwa walishinda kesi hiyo mahakamani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu Mkuu huyo wa mkoa wakati mkutano huo ukiendelea na kumpongeza huku akitoa ufafanuzi wa ubomoaji wa nyumba za watu waliovamia hifadhi ya barabara.

Wananchi:

‘Tulishinda kesi mahakama kuu baada ya hapo tulichukua hatua ya kuvunja nyumba zote kupisha barabara Morogoro.”

Rais Magufuli akampigia simu Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda na kusema haya.

“Nakupongeza sana RC Makonda natamani wakuu wote wa mikoa wangekuwa kama wewe watembelee wananchi kusikiliza kero zao.

“RC Makonda endelea kutembelea wananchi hata majipu yatumbue huko huko.

“Nawapongeza sana DC Ubungo na TANROADS kwa kusimamia sheria vinginevyo tutajikuta siku moja Tanzania hatuna barabara.

“Ndio maana hata ile ofisi iliyokuwa ya TANROADS nilienda kuivunja mwenyewe kwa sababu ilikuwa ndani ya road reserve’

“Wazingatie sheria, kama wanafikiri sheria haifai washauri bunge wabadilishe ili barabara iwe sentimeter 5, ziwe zinapita bajaji tu.

“Nataka niwaeleze ndugu zangu wa ubungo kuvunja kupo palepale kwa sababu tumepata bil 67 za kujenga interchange pale Ubungo.

“Interchange itakayojengwa Ubungo, majengo yatakayokuwa kwenye road reserve yatavunjwa bila fidia hata kama jengo la TANESCO.

“Wananchi wana kero nyingi, viongozi tunajifungia ofisini lakini wewe RC Makonda mwiko huu umeuvunja, una support yangu 100%.

“Ni lazima tuzingatie sheria lakini wananchi kama wanaona wanaonewa waende mahakamani ndio mahali pekee pa kutafsiri sheria.” Alisema Rais Magufuli

Mbali na hivyo, RC Paul Makonda amemuru Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, iliyopo Wilaya ya Ubungo akamatwe na polisi ili akahojiwe kufuatia malalamiko ya wananchi wake kuwa anatumia vibaya ya pesa za wananchi pamoja na kuwanyima fursa ya kufanya mikutano ya maendeleo ya mtaa huo.

Post a Comment

 
Top