KOCHA Mholanzi wa Yanga, Hans va der Pluijm amesema kwamba ataendelea
kupambana hadi tone la mwisho la damu ili kuhakikisha anatetea ubingwa
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga sasa inazidiwa pointi nane na Simba SC wanaongoza Ligi Kuu kwa
pointi zao 35 za mechi 13, baada ya matokeo ya michezo ya juzi. Wakati
Simba ilishinda 1-0 dhidi ya Stand United Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Yanga ilifungwa 2-1 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya.
Na akizungumza jana kwa simu kutoka Mbeya, Pluijm alisema kwamba;
“Sikubali kushindwa hadi mifupa yote isagike. Hiyo ndiyo sera yangu,”
alisema baada ya kuulizwa kama kama bado ana ndoto za kutetea ubingwa.
Post a Comment