Maafisa wawili wa
ngazi za juu nchini Italia wamekanusha vikali ripoti ya shirika la
kulinda haki za binaadam, Amnesty International kwamba polisi nchini
humo wamewanyanyasa wahamiaji wanaotafuta hifadhi wakichukua alama zao
za vidole.
Kundi la kampeni limesema karibu wahamiaji 20
wamelalamika kunyanyaswa, ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwenye shoti za
umeme na kupigwa vibaya.Mkuu wa jeshi la polisi nchini Italia Franco Gabrielli amesema maafisa wa polisi hawakuwahi kutumia njia za kimabavu.
Wakati huo huo mkuu wa kitengo cha uhamiaji katika wizara ya mamabo ya ndani, Mario Morcone amesema alishangazwa na kile alichokiita kuwa ni madai ya uongo.
Alisema kuwa Amnesty ilikusanya ripoti yake mjini London na sio Italia, amabapo wawakilishi wa kamisheni ya juu ya umoja wa mataifa inayoshughulikia wakimbizi walisimamia kilichokuwa kinatokea.
Post a Comment