mwaandishi wetu
MKOA wa Lindi,umebaini
kuwa na watumishi Hewa (171),huku Halmashauri tatu kati ya sita za mkoa
huo,zikiibuka vinara kwa kuwa na idadi kubwa.
Hayo yameelezwa na
mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi alipokuwa anazungumza Ofisini kwake na waandishi
wa vyombo mbalimbali vya Habari, vilivyopo mkoani hapa.
Zambi amesema kutokana
na kuwa na idadi hiyo ya watumishi Hewa, wameweza kuisababishia Serikali hasara
ya Sh,315,223,273/53 kwa ajili ya kulipa mishahara yao.
”Hizi ni takwimu tangu
kuanza kwa zoezi awamu ya kwanza hadi ya tatu,huku Halmashauri ya Manispaa ya
Lindi,ndio inayoongoza kwa idadi kubwa ya watumishi hewa”Alisema Zambi.
Amefafanua kwa kutaja
idadi kwa kila Halmashauri na fedha zilizotumika kulipia mishahara yao kuwa
ni,Lindi Manispaa iliyo na watumishi hewa wapatao (44) na kutia hasara ya Jumla
ya (Sh,64, 363, 403.16),ikifuatiwa na Ruangwa (39) wametafuna (Sh,33,861,037).
Nachingwea (32) kwa
upande wake wametia hasara ya (Sh,108,384, 704.25),Kilwa (29)
(Sh,30,501,515),Halmashauri za Liwale na Lindi vijijini kila moja ikiwa na
watumishi hewa (12) na kutia hasara ya (Sh,71,955, 843.12) wakati Sektarieti ya
mkoa,ikiwa na watumishi hewa watatu, hivyo kutafuna (Sh,6,156771).
Mkuu huyo wa mkoa
amesema katika kuhakikisha fedha hizo zinarudi mikononi mwa Serikali,tayari
Jumla ya Sh,60,685,968/82,zilizokuwa zimelipwa kwa watumishi hao hewa
zimerejeshwa,huku kiasi cha Sh,254,537,304/71,kilichobaki kikiendelea kulipwa
kupitia kwa waliohusika na malipo hayo.
Chanzo:sauti ya kusini
Post a Comment