Wanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) wa vijiji vya Namtumbwa na Mbaya wakiwa ofisi ya mtendaji kata ya Mbaya wakisubiri kuchukua kadi zao za CHF baada ya kuboresha.
Wanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) katika vijiji vya Namtumbwa na Mbaya vilivyopo kata ya Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Liwale wameboreshewa kadi zao kwa kuwekewa picha za utambulisho ambazo zitarahisisha kupata huduma za matibabu bila usumbufu wowote katika vituo mbalimbali.
Zoezi hilo lilianza alhamisi octoba 13 na leo octoba 17 likiwa linaendelea na wananchi wamejitokeza kufuata kadi zao katika ofisi ya mtendaji kata wa kata ya Mbaya iliyopo katika kijiji cha Namtumbwa.
Baadhi ya wanachama wa CHF,Rukia Muharo na Mwanahawa Ng'ombe walizungumza na Liwale Blog walisema mfumo wa kuwewa picha ni mzuri kuliko awali kabla ya kuboresha kuweka picha ilikuwa ukitoka kituo cha afya kimoja kwenda kingine wahudumu walikuwa hawawahamini kama kadi iliyokuwa na jina tu ndio mtu sahihi au ameazima.
Post a Comment