0

Alhamis Oktoba 20,2016-Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Mgambo 141 kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga yaliyoanza Septemba 14,2016 katika kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga.Kati ya vijana 141 waliohitimu mafunzo hayo ya mgambo,wanaume ni 121,wanawake ni 20.
Vijana hao wamepata mafunzo mbalimbali ikiwemo namna ya kutumia silaha mbalimbali,kwata,kuzuia rushwa,zimamoto na uokoaji,usalama wa taifa na mafunzo mengine mbalimbali yanayowesha vijana kuwa wakakamavu na wazalendo kwa nchi yao.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Matiro amewahamasisha vijana hao kutumia vyema mafunzo waliyopata sambamba na kuunda vikundi vya ujasiriliamali ili serikali iweze kusaidia kujikwamua kimaisha.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuzogezea picha 35 wakati mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifunga mafunzo hayo ya mgambo kwa vijana 141.

Wahitimu 141 wa mafunzo ya mgambo kutoka wilaya ya Shinyanga wakiwa katika paredi



Meza kuu: Kushoto ni mshauri wa mgambo wilaya ya Shinyanga Staff Sajent Evarist Nyengu,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,kulia ni mwenyekiti wa mtaa wa Dome katika kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa Naringa,ambaye alijitolea kuwapa nyumba ya kuishi vijana kutoka halmashauri ya Shinyanga waliojitokeza kupata mafunzo ya mgambo yaliyokuwa yanafanyika katika manispaa ya Shinyanga




Wahitimu 141 wa mafunzo ya mgambo wakisubiri kukaguliwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (katikati) akikagua vikosi vya vijana waliohitimu mafunzo ya mgambo kutoka wilaya ya Shinyanga.Kulia kwake ni mshauri wa mgambo wilaya ya Shinyanga Staff Sajent Evarist Nyengu,kushoto ni mkuu wa paredi Charles Busalu akimwongoza mkuu wa wilaya wakati wa ukaguzi wa paredi

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Zoezi la kukagua vikosi likiendelea
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na wageni mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakitoa heshima kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga

Wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakiimba wimbo wa taifa


Wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakitoa heshima kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga



Wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakiongozwa na mkuu wa paredi Charles Busalu wakipita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro

Mkuu wa kikosi namba mbili Manyanda Madirisha akiongoza wahitimu wa mafunzo ya mgambo kupita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga

Kiongozi wa kikosi namba tatu Issack Anthony akiongoza kundi lake


Meza kuu wakiwa wamesimama


Wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakipita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa mwendo wa haraka


Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la tukio
Mshauri wa mgambo wilaya ya Shinyanga Staff Sajent Evarist Nyengu akizungumza ambapo alisema mafunzo hayo yamewafanya vijana hao kuwa wazalendo kwa nchi yao
Mshauri wa mgambo wilaya ya Shinyanga Staff Sajent Evarist Nyengu alitumia fursa hiyo kuwapongeza vijana waliojitokeza kumaliza mafunzo ya mgambo
Wahitimu wa mafunzo ya mgambo wakisoma risala kwa mgeni rasmi.Kushoto ni Jacquiline Kimiti akisoma risala hiyo ambapo alisema watu wengi katika jamii wana imani potofu juu ya mafunzo ya mgambo kwa kuamini kuwa ni mafunzo wanayopewa watu wasio na kazi katika jamii na wengine kutokuwa na elimu juu ya umuhimu wa mafunzo ya mgambo


Meza kuu wakifuatilia risala ya wahitimu wa mafunzo ya mgambo
Msoma risala Jacquiline Kimiti akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro


Wakufunzi wa mafunzo ya mgambo wakijitambulisha
Wakufunzi wa mafunzo ya mgambo wakijitambulisha

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi akizungumza eneo la tukio
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Mgambo Manyanda Madirisha akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kupokea kitambulisho
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Jackline Kibiti akipokea kitambulisho chake baada ya kuhitimu mafunzo ya mgambo
Marwa Magoli akipokea kitambulisho chake
Neema Elihuruma akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kupokea kitambulisho chake

Frank Bara kutoka kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kupokea kitambulisho
Mkufunzi msaidizi wa mafunzo ya mgambo Sajent Geofrey Kamala akizungumza kuhusu mafunzo waliyopata vijana hao 141 kutoka wilaya ya Shinyanga


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo ya mgambo kwa vijana 141,ambapo alisema aliwataka vijana hao kutumia vizuri mafunzo waliyopata ili kulinda raia na mali zao


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema serikali ipo tayari kushirikiana na vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo na kuwataka kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iwasaidie kujikwamua kiuchumi
Vijana waliohitimu mafunzo ya mgambo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwahamasisha vijana hao kutumia mafunzo ya ukakamavu waliyopata kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika jamii


Mkufunzi msaidizi wa mafunzo ya mgambo Sajent Geofrey Kamala akiwasisitiza vijana hao kuzingatia mafunzo waliyopewa-Picha zote na Kadama Malunde

Post a Comment

 
Top