Mradi wa ujenzi wa
reli ya kati nchini Tanzania unatarajiwa kuharakishwa kufuatia
mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na Naibu Waziri wa Biashara wa
China Qian Keming.
Reli hiyo ya kati ni ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na inatarajiwa kuunganisha Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi
Wakati
wa mazungumzo ikulu Dar es Salaam Rais Magufuli alisema serikali
inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda, kwa
mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi katika bajeti ya sasa.
"Sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza
kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali
wa kilomita 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe," alisema Dkt
Magufuli kwa mujibu wa taarifa kutoka ikul..
"Kazi hii tunataka
ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu
umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote
ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani."
Dkt Magufuli alisema mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania
na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba
kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa
Tanzania ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa
mujibu wa taarifa ya ikulu, Bw Qian aliahidi kuwa Serikali ya China
itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli hiyo ya kati.
"Mheshimiwa Rais
Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba
dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma
wataalamu wetu waongeze kasi," alisema.
„Na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa."
Post a Comment