Baadhi ya wafaanyabiashara waliohudhulia semina ya wafanyabiashara leo octoba 5 iliyoendeshwa na mamlaka ya mapato Tanzania katika ukumbi wa Tengeneza (TRA) wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Lengo la semina hiyo kwa wafanyabiashara ni kuongeza uelewa wa kulipa kodi miongoni wa washiriki wa semina kuhusiana na masuala ya kodi kwa wafanyabiashara ili waweze kutekeleza vyema matakwa ya sheria na hivyo kulipa kodi stahiki.
Mgeni rasmi ni Mkuu wa wilaya ya Liwale,Mhe. Saraha Chiwamba aliwakishwa na Kaimu katibu tawala wilaya ya Liwale,ndugu Salumu Chautundu akifungua semina ya wafanyabiashara iliyoendeshwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Chautundu asisiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka usumbusu au kulipishwa fani pia asisitiza kudumisha na kuendeleza kulinda amani wakati wote na pale wanapohofia jambo lolote lisiloeleweka au kuwa mashaka nalo wafuate sheria kwa vyombo husika na kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapata Tanzania (TRA) wilaya ya Liwale,Asimu Ngawembela kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) tawi la Liwale,Juma R. Shaurikum.
Viongozi mbalimbali waliohudhulia kwenye semina hiyo ya wafanyabiashara katika ukumbi wa Tengeneza leo octoba 5 mwaka huu.
Afisa elimu na huduma,TRA,Makao makuu, Julius Mjenga akitoa elimu kwa wafanyabiashara awataka wafanyabiashara wenye sifa wa kutumia mashine za EFD.
TRA inawataka na kuwaomba walipakodi wote wenye sifa wanunue mashine za EFD na kuzitumia kama maelekezo ya serikali yanavyotaka kwa kutoa risiti kwa kila mauzo yote kwa kila mfanyabishara anayofanya kwani ni wajibu wa kila mfanyabiashara kutoa risiti.
Ili kuepuka usumbufu na adhabu ambazo zinaweza kuepukika huna budi kufuata taratibu na sheria zinavyotaka.
TRA inawategemea sana wafanyabiashara katika kufanikisha malengo ya mkoa na kwa Taifa zima,pia Afisa elimu na huduma TRA alibainisha sifa za mfanyabiashara ambaye anatakiwa kutumia mashine ya EFD ni mtu yeyote mwenye mauzo ghafi yanayofikia shilingi milioni 14 kwa mwaka.
Haji Lingindo Katika semina hiyo ya wafanyabiashara aliyeanza kutumia mashine za EFD alitoa changamoto anazokumbana nazo risiti za EFD kufutika kwa kumbukumbuku akiongeza kusema wanapotoa maoni kwa maafisa TRA hawaoni mrejesho wa majibu sahihi kwa wakati.
Hamisi Iluline alisema kwa wafanyabishara wadogo serikali ilitangaza mashine zitagawia bure lakini sasa wanaambiwa wanunue jambo ambalo linawafanya kushindwa kufahamu ukweli sahihi juu ya nani anapaswa kununua mashine ya EFD kati ya mfanyabiashara mdogo au serikali.
Kasimu Oni na Musa Mkoyage walisema wafanyabishara wengi wilayani Liwale hawana elimu ya biashara na wameiomba TRA kutoa elimu mara kwa mara kwa wafanyabiashara.
Post a Comment