TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MUHTASARI WA MKATABA.
1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji” kwa muhtasari wa maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano Mkuu wa Young Africans Sports Club uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016 ulitambua kuwa Young Africans Sports Club (anayejulikana hapa kama “YANGA”):
1.1 KWA KUWA, Timu ya Soka ya Mmiliki ni kongwe na yenye mafanikio
kuliko timu ya soka nyingine zilizoko katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, yenye thamani kubwa kiutamaduni na kwa urithi wa Taifa, licha
ya jitihada zake zote, inakabiliwa na changamoto za kifedha katika
kuiendesha timu yake ya mpira wa miguu, kwa kuwa na usajili mdogo wa
uanachama, ukosefu wa mapato, ya ada za Wanachama, mifumo isiyo na
ufanisi ya kiuendeshaji, kushindwa kujipatia kipato cha kibiashara
kutoka katika hati miliki na nembo za kibiashara za Timu ya Soka ya
YANGA kutoweza kujiendesha kibiashara na Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Tanzania (TFF)- ambalo kwa mfululizo linasababisha YANGA kuiendesha
Klabu yake kwa hasara na kuwa tegemezi kutoka kwa michango ya wahisani
na kwa mikopo na kukabili changamoto hizi; na Mkutano wa Wanachama wa
YANGA tarehe 6 Agosti 2016 uliazimia kugeuza hali hii kwa kukodisha Timu
ya Soka ya YANGA ambayo ilikuwa inajiendesha kwa hasara na mapato
madogo kupitia nembo yake na hakimiliki yake (jina na nembo) kwa muda
wa Miaka (10), ili kuikinga Klabu kutoendelea kujiendesha kihasara
katika kipindi cha Miaka (10) ya ukodishwaji, ijipange kiuwezo ili Timu
ya Soka ya Mmiliki na hakimiliki za jina lake na nembo zitakapo
rejeshwa baada ya kukodishwa kwa kipindi cha Miaka (10), YANGA itakuwa
inaweza kujiendesha yenyewe na iwe na uwezo wa kifedha na iweze
kushindana kikamilifu katika shughuli za mpira wa miguu.
2. Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji”) ni Kampuni
iliyoundwa ili iweze kuingia katika Mkataba na YANGA ili iweze kutimiza
malengo ya Klabu kama yalivyo azimiwa katika Mkutano wa Wanachama wa
YANGA uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016.
3. Baraza la Wadhamini wa Young Africans Sports Club baada ya mazungumzo
na Mkodishwaji linapenda kuwafahamisha Wana YANGA kuhusu mambo muhimu
yaliyomo kwenye Mkataba Huu ulioingiwa kwa kuzingatia na kwa haki miliki
kutolewa kwa Mkodishwaji kwa njia ya Mkataba Huu, kwa kukodisha Timu ya
Soka ya Mmiliki na haki zake zote, mamlaka na majukumu yote, jina lake
na nembo kwa ajili ya kutumika kiamani na kibiashara katika kuziendesha
shughuli za Timu ya Soka ya Mmiliki bila ya kuwa na kuingiliwa katika
muda wa Mkataba huu kwa muda wa Miaka (10) kuanzia Tarehe ya Ufanisi ya
1 Septemba, 2016, ila kama utasitishwa kabla kufuatana na matakwa ya
Mkataba:
3.1 Mkodishwaji atailipia YANGA deni la Shilingi bilioni kumi na moja na
milioni mia sita na sabini na sita tu (Tshs. 11,676 billioni)
inayodaiwa kama Mmiliki na Mkopeshaji mmoja.
3.2 Mkodishwaji atailipa YANGA Tshs 100 millioni kwa mwaka ambayo YANGA
itawekeza kiwango kisichopungua (90%) ili kuimarisha mtandao wa Matawi
yake.
3.3 Mkodishwaji atailipa YANGA katika mwaka wa fedha wowote ule kukiwa
kuna faida ya fedha taslim ya asilimia 25% fedha ambayo YANGA itaitumia
kujenga uwanja wake wa mpira.
3.4 Mkodishwaji atalipa hasara za uendeshadji zilizoko katika Mkataba kutoka kwenye mfuko wake bila ya kuweka madai kwa YANGA.
3.5 Mkodishwaji ataanza kuwekeza kwa vitega uchumi kuanzia siku (90) ya
Mkataba katika mafunzo na vifaa, ambavyo kutakuwepo kiwanja cha mafunzo
ya mpira katika sehemu atakayo ona inafaa kwake yeye Mkodishwaji.
3.6 Mkodishwaji atahakikisha kuwa majukumu yote ya kifedha ya Timu ya
Soka ya YANGA ikijumlishwa ada ya usajili zinazotakiwa kuanzia Tarehe ya
Ufanisi na majukumu mengine ya siku zijazo yanalipwa kulingana na
mahitaji ya YANGA mapema kutoka kwenye mfuko wa Mkodishwaji.
3.7 Mkodishwaji atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya YANGA haitamaliza
chini ya nafasi nusu mwisho wa msimu wa ligi ya Tanzania Premium League
wakati ikiwa ndani ya kipindi cha Mkataba.
3.8 Mkodishwaji atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya Mmiliki iliyokodishwa
katika kipindi cha misimu 3 mfululizo itamaliza ikiwa ni mshindi wa
nafasi 2 za juu kwenye Tanzania Premium League.
3.9 Mkodishwaji, kwa kila mwaka atafadhili mashindano ya mpira katika
mfumo utakao amuliwa na yeye Mkodishwaji kwa Timu ya Soka kwa vijana
wenye umri chini ya miaka (18) na kila Tawi la Wanachama wa YANGA
litaalikwa kutuma timu yake kushiriki katika shindano hilo.
3.10 Mkodishwaji atakabidhi kwa YANGA tuzo zozote au Nishani yoyote Timu
ya Soka ya Mmiliki ikipata, na kuitaarifu YANGA kabla, pale itakapo
wezekana, ili YANGA iweze kumteua mwakilishi wa kupokea tuzo hiyo kwa
kuitambua Timu ya Soka ya Mmiliki.
3.11 Mkodishwaji ataingia katika Mikataba yote ya ufadhili au mikataba yaleseni kwa kuitisha zabuni kupitia Zabuni za Umma.
3.12 Mkodiswaji ataunda na kuiendesha Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana kulingana na kanuni na miongozo ya TFF.
3.13 YANGA itateua moja kati ya kampuni Tano (5) za Ukaguzi Kongwe
Duniani wa Mahesabu zije kukagua kwa kila mwaka hesabu za Mkodishwaji
kuhakikisha hakuna ubadhirifu.
3.14 YANGA itakuwa na haki ya kipekee kabla ya Tarehe ya Ufanisi wa
Mkataba huu kiwango chochote ambacho kinastahili kupata kutoka TFF,
ikiwemo Mkataba wa Azam TV ambao unakadiriwa kuwa shilingi milioni mia
tatu (300,000,000) kwa matangazo ya msimu uliopita, mikataba ya
ufadhili, madeni ambayo haijalipwa, fedha za zawadi, VAT kutoka TFF na
fedha zingine zote zitapewa umuhimu wa nafasi ya kwanza katika matumizi
ya kukamilisha majukumu ya zamani ya Timu ya Soka ya YANGA ambayo
yalijilimbikiza na hayakuwa wamelipwa.
3.15 Mkataba huu utakapo fikia ukomo, YANGA itakuwa na haki ya kurejesha kile ilichokikodisha.
4. Ilikubaliwa kwamba YANGA:
4.1 Itajitahidi mnamo kipindi cha miaka miwili ya Mkataba itakuwa na
Wanachama hai 100,000 na kwa kila Wanachama 100,000 itateua Mjumbe mmoja
kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Mkodishwaji.
4.2 Itafanya kila juhudi ya kuongeza ardhi inayohitajika katika Makao
Makuu yake yaliyopo mtaa wa Twiga ili iweze kujenga uwanja wa mpira
unaofaa, ambao Mkodishwaji atawajibika kuchezea michezo yake ya Timu ya
Soka ya YANGA, kwa masharti yatakayo kubaliwa baina ya Pande zote za
Wahusika.
4.3 Itakuwa na haki katika wakati wowote ule ndani ya kipindi cha
Mkataba kusitisha Mkataba ili mradi imfidie Mkodishwaji hasara zote za
nyuma, ilipe malipo yote yaliyofanywa kwa YANGA na Mkodishwaji,
inachukua mali zilizowekezwa na Mkodishwaji na kumfidia mapato ya siku
zijazo – zote, hizi zikiwa zimetathminiwa na moja ya Kampuni za Wakaguzi
(5) Kongwe Duniani.
4.4 Ikiwa Mkodishwaji atakarabati au atatumia mali yoyote ya YANGA
ataifidia YANGA kwa masharti yaliyokubaliwa kwa masharti tofauti ya
Mkataba Huu.
4.5 Mkodishwaji atakuwa na haki ya kipekee ya kiwakilishi (Exclusive
Power of Attorney) kwa YANGA kufanya mikataba na TFF, CAF & FIFA kwa
niaba ya YANGA bila ya kuingiliwa kati na YANGA lakini anapaswa atoe
taarifa kuhusu uwakilishi huo kwa Baraza la wadhamini, kuanzia Tarehe ya
Ufanisi wa Mkataba Huu pamoja na haki ya uwakilishi wa YANGA kwa: i)
kuunda Kamati zinazohitajika na TFF, CAF na FIFA kuiendesha Timu ya Soka
ya Mmiliki iliyokodishwa ii) kusajili au kulisimamisha benchi la ufundi
na wachezaji kutoka Timu ya Soka ya YANGA, iii) Kuwa Msemaji Mkuu wa
Timu ya Soka ya YANGA kwa Umma.
5. KUFUNGA.
5.1 Bodi ya Wadhamini wa YANGA inapenda kumshukuru Bw. Yusuf Mehbub
Manji kwa kupendekeza masharti bora kuliko yale yaliyoazimiwa na
kukubalika kwa Wanachama kwa manufaa ya YANGA, na tunampigia saluti
uchangiaji wake usio na choyo kwa manufaa ya YANGA.
5.2 Tungependa kuufahamisha Umma kwamba Bw. Yusuf Mehbub Manji ametaka
kujiuzulu kutoka Uenyekiti wa Klabu ili kuepusha mgongano wa kimaslahi,
lakini tumelikataa ombi lake hili – kwa vile nafasi ya Mwenyekiti wa
Klabu, Wanachama wameonyesha kwa kura zao kuwa wana imani na uongozi
wake, kwa vile wakati wa majadiliano, haweki maslahi yake binafsi juu ya
yale ya Klabu, lakini anajaribu kadri iwezekanavyo kuisaidia Klabu
kuweza kujitegemea kifedha haraka iwezekanavyo ili kuendelea kushindana
katika mpira wa miguu kwa kiwango cha juu zaidi, hapohapo akilinda
urithi wa Klabu na utamaduni – sifa ambayo tunaihitaji katika Mwenyekiti
wa YANGA na kama akijiuzulu kutoka kwenye Klabu, tutakuwa tumempoteza
kiongozi mwenye uzoefu na maadili ya hali ya juu wakati tunapofanya
mageuzi ya YANGA.
Tunachukua fursa hii kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki kuwa kuna
kazi nyingi kwa faida ya YANGA ambazo Bw. Yusuf Manji anazifanya ambazo
hazionekani mbele ya jamii: kitu ambacho kinahitajika katika Klabu.
Tunapenda kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki wawe waangalifu na maneno
yao, kwa vile kauli za maneno ya matusi zinaumiza na zinawavunja moyo
viongozi kama Bw. Yusuf Manji ambao tunafahamu hawagombei nafasi za
Uongozi wa ndani ya Klabu, kwa sababu wanachukizwa na kutukanwa na
Wanachama na hivyo basi, tunawapa mawaidha Wanachama, kwa manufaa ya
Klabu watoe maoni yao kuhusu mambo ya soka na utawala wa soka, na siyo
kwa watu na familia zao.
5.3 Sasa tunapenda kuwafahamisha Wanachama wa YANGA na Wapenzi wa YANGA
kuwa kilichotiwa saini baina ya Pande Zote ni Mkataba ya kihistoria, na
kama yakitekelezwa na pande zote mbili, YANGA itanufaika kwa hali ya juu
mno kutokana na mazingatio na ushahidi iliyoupata kupitia Baraza lake
la Wadhamini kwenye Mkataba wa ukodishwaji.
5.4 Mwisho, tumeombwa na Bw. Yusuf Manji tutangaze hadharani Mkataba
Huu, hata hivyo bado tunajadiliana kama kutangazwa huko kutakuwa kwa
manufaa ya Klabu, kwa kuwa, kwa upande mmoja ni vema kuwa na uwazi,
lakini kwa upande mwingine washindani wa Klabu yetu wataiga Mkataba
wetu kwa manufaa yao.
YANGA
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO
………………………………………….
BODI YA WADHAMINI WA YANGA
BODI YA WADHAMINI WA YANGA
Post a Comment