0
Mchezaji wa timu ya Sido fc,Haikosi Mpwate (kushoto) akiwa na mpira akijaribu kutoa pasi ili kuweza kusawazisha magoli.






Leo asubuhi na mapema katika uwanja wa halmshauri ambako unatumika kuchezea michezo yote ya ligi daraja la nne kulikutwa kumemwagwa mchele hali ambayo si ya kawaida na baadae mchele huo kulipotea ambapo leo kulikuwa na mchezo wa watani wa jadi kati ya timu ya Sido fc dhidi ya New generation timu ambazo zenye mashabiki wengi sana.

 Matokeo ya leo octoba 27 katika mchezo wa ligi daraja la nne uliwakutanisha watani wa jadi kati ya timu ya Sido fc dhidi ya New generation na kuambulia kila timu kuvuna pointi 1 baada ya kutoka sare ya kufungana goli 2 kwa 2.

Mchezo huo ulitumua vumbi katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo katika kipindi cha kwanza timu ya New generation ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu mapema namo dakika ya 14 na 29 magoli yote yakifungwa na Omari Matwiko na magoli hayo kudumu mpaka 45 za kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili timu ya Sido fc iliweza kusawazisha magoli yote mawili katika dakika ya 61 lililofungwa na Masudu Mbwana na dakika ya 64 Hasani Samora alipachika goli la pili na kulazimisha kutoka kwa sare ya magoli 2 kwa 2.

Post a Comment

 
Top