0


 Kula chumvi vyingi kunaelezwa kusababisha madhara mengi kwa afya ya binadamu.

Chumvi inapandisha shinikizo la damu. Shinikizo la juu la damu (presha) ni sababu kubwa ambayo husababisha la kiharusi(stroke),kusimama kwa moyo,shambulio la moyo na magonjwa mengine mengi ya moyo kote duniani.

Kunaushahidi wa kutosha wa kitafiti kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ulaji wa chumvi kwa wingi na kansa ya tumbo, osteoporosis(hali ya mifupa kuwa rahisi kufunjika na tete kutokana na upungufu wa Kalsiamu  na vitamini D),mawe ya figo,ugonjwa wa figo na mwili kupoteza maji.

Chumvi inaweza pia kuongeza dalili za pumu, magonjwa na ugonjwa wa kisukari.
Kiasi kidogo cha chumvi ni muhimu kwa afya zetu.Watu wazima wanahitaji chini ya gramu1(kijiko kidogo cha chai) kwa siku na watoto wanahitaji kidogo zaidi.

Watu wengi tunakula zaidi ya gramu 8 kwa siku za chumvi ambayo ni nyingi maradufu ya kiwango cha juu kinacho shauriwa cha gramu 6 kwa siku hivyo kutuweka katika hatari zaidi ya kukumbwa na magonjwa yaliyotajwa.

Habari njema ni kwamba kupunguza ulaji wa chumvi yako unaweza kupunguza shinikizo la damu na hatari ya magonjwa mengi. Ukiweza kupunguza na kufikia gramu 3 kwa siku basi unajiweka katika nafasi nzuri kiafya.

Shinikizo La Damu(Presha)

Shinikizo la damu ni kiasi cha mkandamizo ambao damu inaweka katika kuta za mishipa ya damu wakati moyo unaposukuma damu mwilini.

Mambo fulani kama vile kuwa na uzito mkubwa, ukosefu wa mazoezi, na hususani kula vyakula nyenye chumvi nyingi vinaweza kuongeza shinikizo la damu yako, na kusababisha mashambulizi ya moyo na kiharusi.

Kiharusi Au “Stroke”
Kiharusi kwa kawaida hutokea wakati damu inaposhindwa kupelekwa katika ubongo ambako kuna sababisha kupunguza mtiririko wa oksijeni kwenye ubongo, na kusababisha seli kufa.

Kuna aina kuu mbili za kiharusi
1. Ischemic Stroke: Hutokea wakati mishipa ya damu inapokuwa imefungwa kupeleka damu kwenye ubongo
 2. Hemorrhagic Stroke: Hutokea wakati mishipa ya damu katika ubongo inapopasuka na kusababisha damu kuchanganyika na ubongo
Shinikizo la damu ni moja ya sababu kubwa ya kiharusi na chumvi ni sababu kubwa ambayo inachangia shinikizo la damu hivyo chumvi ni sababu kubwa ya kiharusi.

Kiharusi ni mojawapo ya magonjwa yanayokuja na umri mkubwa lakini kinaweza kuepukika kwa kuzui shinikizo la damu kwa njia ya kupunguza ulaji chumvi, mazoezi na kula vyakula vyenye kuleta afya njema.

Ugonjwa Wa Moyo
Ugonjwa wa moyo ni neno linalotumika kuelezea kile kinachotokea wakati ugawaji wa damu katika moyo unapopungua au kufungwa na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi sawa sawa.

Watu wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa moyo duniani ,inaaminika takribani watu 300,000 wanakufa kwa mshtuko wa moyo kila mwaka.

Shinikizo la damu linachangia magonjwa ya moyo kushindwa kufanya kazi. Shinikizo la muda mrefu linasababisha mishiba ya damu kuwa myembamba na kushindwa kupeleka damu ya kutosha kwenye moyo na hivyo kufanya moyo kusukuma kwa nguvu zaidi na hatimaye kuchoka.

Hivyo ukipunguza chumvi unaweka shinilizo la damu chini hivyo kuepuka magonywa ya moyo.

Kansa Ya Tumbo
Ulaji wachumvi nyingi katika chakula kunaongeza hatari ya kansa ya tumbo.

Watafiti wa afya waneleza kuwa karibu robo ya kesi mpya za kansa ya utumbo kila mwaka yanaweza kuhusishwa na chumvi.

Bakteria Helicobacter pylori (H. pylori) ni hatari kubwa kwa sababu husababisha uvimbe wa tumbo ambayo kwa husababisha vidonda vya tumbo na kansa ya tumbo.

H.Pylori katika tumbo siyo lazima asababishe uharibifu, lakini chumvi inauwezo wa kuharibu ngozi ya juu ya tumbo, na kuifanya ishambuliwe na bacteria H. Pylori na kusababisha madhara.

Inasemekana wanaume wapo katika hatari kubwa zaidi kuliko wanawake kibayolojia.

Ugonjwa Wa “Osteoporosis“
Osteoporosis ni hali ambayo husababisha kukonda kwa mifupa,na kuifanya iwe rahisi kuvunjika au kukatika.

Madini ya Kalsiamu katika mwili huhifadhiwa katika mifupa. Chumvi ya kupita kiasi katika chakula inaweza kusababisha kalsiamu kupotea katika mifupa na kutoka katika mkojo, na kufanya mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kwa urahisi.

Uzito Mkubwa Wa Mwili Na Kitambi
Idadi kubwa ya watu wengi hasa mijini wana uzito wa kupindukia kutokana na mtindo wa maisha ya kutofanya kazi za kutumia nguvu za mwili.

 Uzito mkubwa wa mwili unahusishwa na matatizo mbalimbali ya afya kama vile shinikizo la damu,ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo na matatizo ya usingizi.

Chumvi haisababishi ongezeko la uzito ila inakufanya upate kiu, na kukusababisha kunywa maji zaidi, au vimiminika vyenye sukari kama soda na juisi ambazo zinaweza kusababisha kuongezeka uzito.

Mawe Ya Figo Na Ugonjwa Wa Figo
Mawe ya Figo ni mojawapo ya matatizo ya watu wengi,tatizo hili linasababishwa na kalsiamu kukusanyika katika figo.

Ulaji wa chumvi nyingi na shinikizola damu husababisha kalsiamu kukusanywa na figo kwenda kwenye mkojo.

Mkusanyiko wa kalsiamu katika figo hatimaye hutengeneza jiwe ambalo baadae husanbabisha figo kushidwa kufanya kazi ipasavyo.

 Tatizo La Kutunza Maji Mengi Mwilini
Ulaji wa chumvi unatufanya kuhifadhi maji, hadi lita 1.5 mwilini na kusababisha kuwa na damu nyingi na nyepesi kama unakunywa maji mengi

Unapokula chumvi nyngi,sodiamu hujilimbikiza nje ya seli yako ambayo huhitaji uwepo wa maji katika seli.

Kama ulaji wa sodiamu uko juu, figo hukata kiasi cha maji yanayopelekwa kwenye mkojo toka mwilini uli yasaidie kurekebisha sodiamu iliyozidi. Hii inasababisha kuongezeka kiasi cha damu mwilini kutokana na maji yanayobakizwa na kusababisha uvimbe, katika sehemu mbalimbali za mwili.

Upungufu Wa Maji Mwilini
Kula chumvi nyingi kunasababisha ongezeko la sodiamu mwilini hivyo mwili unahitaji maji zaidi ili kuisukuma kwenda katika mkojo hivyo kupungukiwa maji.

Kama si mnywaji wa maji mengi,figo zitatumia maji yote mwilini ilikuondoa sodiamu iliyozidi.

Unaweza hatimaye kuhisi kiu kali, kichefuchefu, kizunguzungu, maumivu ya tumbo, kutapika na kuharisha kutokana na sodiamu iliyozodi kushindwa kuondolewa.

Pumu (Asthma)
Ulaji wa chumvi nyingi hakusababishi pumu, lakini baadhi ya utafiti umeonyesha kwamba inaweza kuchochea dalili.

Kama mtoto wakoinakabiliwa napumu,kupunguzaulaji wa chumvi kunaweza kuwa na manufaa.

Ugonjwa Wa Kisukari
Mojawapo ya magonjwa hatari yanayoua sasa hivi ni kisukari.

Kisukari kimekuwa ni tatizo kubwa. Angalau katika kila familia kuna mgonjwa mmoja wa kisukari na idadi inaongezeka kila siku.

Chumvi inaweza kuongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari kwa kuongeza shinikizo la damu.

Watu ambao tayari wanaugonjwa wa kisukari unawezapia kufaidika nakula chumvikidogoili kuweka shinikizo la damu chini.


Kupunguza Matumizi Ya Chumvi Na Madhara Ya Kula Chumvi Nyingi:
Anza kujenga tabia ya kula chumvi kidogo, usiweke chumvi mezani. Punguza kiasi cha chumvi unayoweka katika chakula chako kidogokidogo mpaka utakapozoea.

Mwili wa binadamu unajifunza mambo kwa mazoea.  Ukiweka tabia ya kula chumvi kidogo baada ya miezi kadhaa utafanikiwa na  utakuwa umejiepusha  na madhara ya kula chumvi nyingi.

Post a Comment

 
Top