Mgeni rasmi ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,Justin Monko
Rukia Kangungu akisoma risara kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Mihumo katika risara hiyo walibainisha moja ya changamoto ni utoro kwani darasa hilo walianza wakiwa jumla ya wanafunzi 65 ikiwa wavulana 31 na wasichana 34 lakini mpaka wanahitimu kidato cha nne darasa hilo likiwa na idadi ya wanafunzi 24 kati yao wavulana 10 na wasichana 14.
Rukia Kangungu akikabidi risara kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,Justin Monko
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Mihumo,David J. Ulomi akisoma risara na kueleza baadhi ya changamoto na kuomba kutatuliwa kwa changamoto hizo ili kuweza kuleta ufasi shuleni hapo.
Mwalimu mkuu akipeana mikono na mkurugenzi wa halmashauri ya wialya ya Liwale mara baada ya kukabidhi risara
Shule ya sekondari ya Mihumo iliyopo wilaya ya Liwale mkoani Lindi inafanya vizuri kitaaluma ikiwa ufaulu wake unaongeza kupanda kwa kila mwaka kuanzia matokeo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Taarifa hiyo ya maendeleo ya shule ilisomwa na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ,David J. Ulomi kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa halmashuri ya Liwale,Justin Monko kwenye maafali ya kidato cha nne yaliyofanyika octoba 15 mwaka 2016 shule hapo.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2008 ikiwa na jumla ya wanafunzi 80 ikiwa wavulana 40 na wasichana 40 ikiwa na mwalimu mmoja na baadae aliongezeka mmoja na kuwa na idadi ya walimu wawili sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 165 ambao wavulana ni 81 na wasichana 84,walimu 13 wanaume 9 na wanawake 4.
Shule ilianza ikiwa na madarasa 3 na sasa ina madarasa 5 yaliokamilika na madarasa 2 ambayo hayajakamilika,shule hiyo ina majengo ya maabara 3 ikiwa maabara ya Physics,Biology na Chemistry na jengo moja la bweni la wasichana ambalo halitumiki kutokana na kutokabidhiwa kwa shule huku bweni hilo likiwa halina vitanda.
Matokeo ya kidato cha pili yalikuwa kikanda kwa kanda ya kusini ilikuwa inajumisha mikoa ya Lindi na Mtwara kama ifuatavyo mwaka 2010 ilishika nafasi ya 19 kati ya 225,2011 nafasi ya 156 kati ya 234,mwaka 2012 nafasi ya 27 kati ya 243,mwaka 2013 nafasi ya 141 kati ya 257,mwaka 2014 walifanya mtihani 25 na wote walifaulu na mwaka 2015 waliosajiliwa 24 waliofanya mtihani 19 na walifaulu 17.
matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2012 kimkoa 16 kati ya 43 kitaifa nafasi ya 498 kati ya 754 na mwaka 2013 kimkoa nafasi ya 28 kati ya 52 kitaifa nafasi 944 kati 1099,mwaka 2014 kimkoa nafasi ya 38 kati ya 88 kitaifa nafasi 1135 kati 2097 na mwaka 2015 kimkoa nafasi ya 12 kati ya 62 kitaifa nafasi 635 kati 1162.
Licha ya shule ya Mihumo kufanya vizuri kitaaluma lakini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa njia moja au nyingine zimesababisha kurudisha taaluma nyuma.
Mwalimu mkuu, Ulomi alibainisha baadhi ya changamoto ikiwa tatizo la maji ya kudumu shuleni hapo na kupelekea baadhi ya wanafunzi kuacha shule,utoro sugu unaopelekea wanafunzi kuacha shule kwa kutokuwa na sababu za msingi,ukosefu wa umeme pamoja ya kompyuta ya kurudishia mitihani kwani kipindi cha maandalizi ya mtihani hulazimika kutumia gharama kubwa na upungufu wa nyumba za walimu kwani ina nyumba za waloimu 5 ikiwa zilizokamilika ni 2 tu.
Kwa upande wa mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya Liwale,Justin Monko akijibu baadhi ya changamoto alisema moja ya changamoto kubwa wilayani Liwale ni upungufu wa madarasa. Pia katika tatizo la maji alisema ataboresha miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza kipato kwa wananchi wa kijiji cha Mihumo.
Tatizo la mabweni wazazi wanatakiwa washiriki kikamilifu kwa kushilikiana na wadau katika kufanikisha ukamilishaji wa mabweni ili wanafunzi waweze kuyatumia na kuleta motisha kwa wanafunzi na amewataka wazazi kuwekeza kwenye elimu kwani upande wa elimu kuna tija kubwa na ndio msingi muhimu katika maisha.
Monko aliwata wahitimu pamoja na wazazi kujifunza kwa waliofanyikiwa ili nao kuweza kufanyikiwa pia
Katika hatua nyingine mkurugenzi aliweza kuendesha zoezi la alambee ya kuchangia fedha ili kuweza kutatua baadhi ya changamoto shuleni hapo kwa kununua kipande cha keki ambapo zoezi hilo liliungwa mkono na wazazi walioudhulia kwenye mahafari hayo ambapo waliweza kufanyikiwa kukusanya jumala ya fedha taslimu shilingi 361000 na ahadi kiasi cha shilingi 45000.
angalia baadhi ya picha za matukio
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,Justin Monko akiwahutubia wazazi,walezi na wahitimu wa kidato cha nne kwenye maafali katika shule ya sekondari Mihumo.
Igizo lililoigiwa mzee akiuza mbogamboga ili apate fedha aweze kumsomesha mwanae hatamaye mwanae alisoma alifaulu na alipata kazi baadae mtoto akamdharau wazazi hatimae mtoto akafirisika kutokana na rahani ya wazazi
Burudani nazo zilikuwepo ambazo iliweza
kuburudisha zikiwa zimebeba ujumbe mbalimbali ikiwa baadhi ya ujumbe
UKISOMA NA UKIFANYIKIWA HAUTAKIWI KUWADHARAU WAZAZI WALIOKUSOMESHA KWA
SHIDA MPAKA UKAPATA KAZI.
Burudani nazo zilikuwepo ambazo iliweza
kuburudisha zikiwa zimebeba ujumbe mbalimbali ikiwa baadhi ya ujumbe
UKISOMA NA UKIFANYIKIWA HAUTAKIWI KUWADHARAU WAZAZI WALIOKUSOMESHA KWA
SHIDA MPAKA UKAPATA KAZI
Burudani nazo zilikuwepo ambazo iliweza kuburudisha zikiwa zimebeba ujumbe mbalimbali ikiwa baadhi ya ujumbe UKISOMA NA UKIFANYIKIWA HAUTAKIWI KUWADHARAU WAZAZI WALIOKUSOMESHA KWA SHIDA MPAKA UKAPATA KAZI
wahitimu wa kidato cha nne
mkurugenzi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wahitimu wa kidato cha
nne na zawadi maalum kwa walioweza kufanya vizuri katika masomo
mbalimbali
mkurugenzi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wahitimu wa kidato cha
nne na zawadi maalum kwa walioweza kufanya vizuri katika masomo
mbalimbali
mkurugenzi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wahitimu wa kidato cha
nne na zawadi maalum kwa walioweza kufanya vizuri katika masomo
mbalimbali
mkurugenzi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wahitimu wa kidato cha nne na zawadi maalum kwa walioweza kufanya vizuri katika masomo mbalimbali
Mkurugenzi akiendesha zoezi la ukataji wa keki kwa lengo la alambee
Afisa elimu akichangia fedha katika jitihada ya kuweza kufanyikisha kutatua changamoto ili wanafunzi wawezi kusoma katika mazingira bora
Mkurugenzi akimlisha keki ambayo aliweza kuwanunulia wahitimu wote keki vipande vyenye thamani ya shilingi 40000
wazazi,walezi pamoja na wadau mbalimbali wakionga mkono zoezi la alambee ya kuchangia fedha ili kuweza kutatua baadhi ya changamoto ndogondogo shuleni hapo
wakipokea alambee kutoka kwa watu mbalimbali walioungana kuchangia fedha ili kuweza kutatua changamoto za shuleni hapo ili kuweza kuboresha huduma mbalimbali
wazazi,walenzi pamoja na wageni waalikwa waliohudhulia maafari
wanafunzi wakifuatilia mambo mbalimbali kwenye maafali ya kidato cha nne
Picha ya pamoja ya wahitimu na viongozi mbalimbali walioudhulia kwenye maafari katika shule ya sekondari ya mihumo
Post a Comment