Michezo miwili ya kirafiki ilipigwa katika viwanja viwili tofauti hapa wilayani Liwale mkoani Lindi.
Mchezo wa kwanza timu ya Nangando fc iliikaribisha Sido fc
na kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1 mchezo uliopigwa uwanja wa
wilaya ya Liwale.
Moli la timu ya Nangando fc lilifungwa na Erick Mnape katika dakika ya 32 huku goli la kusawazisha la Sido fc lilifungwa na Hasani Kichele namo dakika ya 40.
Mchezo kati ya Liwale Day fc dhidi ya timu ya maafande Polisi fc mchezo uliochezwa uwanja wa wshule ya sekondari Liwale day octoba 14 2016.Timu iliyovaa njano ni timu ya polisi fc na timu iliyovaa uzi mwekundu ni Liwale day angalia jinsi ya ukabaji ulipokuwa uwanjani
Mchezo wa pili ulipigwa uwanja wa shule ya Liwale day kati ya timu ya shule ya sekondari ya Liwale high school dhidi ya maafande polisi fc mchezo uliowatoa jasho polisi fc kwa kulazimisha sare ya goli 1 kwa 1.
Moli la timu ya Liwale day fc lilifungwa na Rabini Issa
katika dakika ya 40 huku goli la kusawazisha la Polisi fc lilifungwa na Shara namo dakika ya 70.
Post a Comment