JESHI la Polisi nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa
ya kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi
katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705, Katika
matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa
kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393.
Hayo yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa
Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es
Salaam leo, tarifa hiyo imeeleza kuwa kuzipuuza sheria za nchi
zilizopo na wakati mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi
yao kufikia hatua ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa
vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya
mhalifu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za
kisheria kwa kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia
za kujichukulia sheria mkononi.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi
mkubwa katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya
kujichukulia sheria mkononi na badala yake wananchi kuendelea kutii na
kufuata sheria za nchi zilizopo.
Post a Comment