0
Mkuu wa Wilaya Nachingwea Rukia Muwango anawatangazia wananchi wote Wilaya ya Nachingwea kushiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yatakayofanyika katika uwanja wa sokoine Mnamo octoba 14, 2016.

Maadhimisho yataanza kwa maandamano kuanzia saa 12.30 asubuhi, yakiongozwa na Mhe. Godfrey Zambi Mkuu wa Mkoa Lindi, maandamano yataanzia ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuelekea uwanja wa sokoine. 

 Itakuepo pia Michezo mbalimbali kama vile ,kuvuta kamba,kukimbiza kuku, mashindano ya kula mkate na kunywa soda kwa mwendo kasi, kunywa Maziwa ya moto kwa kasi, kukimbia kwa Gunia kukimbiza kuku, Kucheza Bao.

Aidha, kutakuwa na zoezi la kutambua afya zetu kwa kupima BURE :-
●VVU
●Kisukari
●Shinikizo la damu
● *Uchangiaji* *wa* *Damu*
●Kutakuwa pia na huduma za ufunguaji wa Akaunti kutoka katika taasisi za kifedha na
●Elimu ya mfumo mpya wa ukusanyaji na uuzaji wa Korosho msimu huu 2016/2017
Watumishi wote wa Umma na Sekta binafsi, wananchi wote mabibi na mabwana mnakaribishwa kushiriki maadhimisho haya Muhimu.

Vazi la maandamano ni lolote rangi nyeusi au nyeupe kwa aliyekuwa nalo.

Post a Comment

 
Top