Barabara ya mradi wa mabasi yaendayo haraka katika kituo cha
Kisutu,kilichopo katika Makutano ya barabara ya Libya na Morogoro,Mtaa
wa Mtendeni,Kata ya Kisutu,Manispaa ya Kinondoni,Dar Es
Salaam,inaendelea kuchimbika kufuatia sababu mbalimbali ikiwemo
kinachoonekana kama mamlaka husika kuzembea ama kutochukua hatua stahiki
kunusuru hali ilivyo mahala pale.
Chanel Ten,imeshuhudia Madereva wa magari ya mwendo wa haraka wanaopita mahala hapo namna wanavyopita kwa taabu wakijitahidi kudhibiti mwendo mahala hapo, huku wengine wakichepuka kidogo hivyo kusababisha kingo za barabara katika eneo hilo nazo kuendelea kuathirika.
Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya madereva taksi wa kituo cha Kisutu,wanaoegesha pembeni mwa makutano ya barabara hiyo ya Libya na Morogoro,wakiwemo waenda kwa miguu wanaotumia barabara hiyo kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam,kuhusiana na kuchimbika kwa barabara katika eneo hilo.

Post a Comment