Mabingwa wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati timu ya Azam FC, Jana octoba 2 imeshindwa tena kuvuna point 3 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania
Bara uliopigwa katika dimba la Chamazi, Dar es Salaam, kwa kulazimishwa
sare ya 2-2 na Ruvu Shooting.
Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Fully Maganga katika dakika ya 8 ya mchezo, na Azam kufanikiwa kusawazisha dakika ya 29 kupitia kwa Baptista Mugiraneza kwa kichwa akimalizia kona ya Mcha na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1 .
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kutawala zaidi mchezo na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 70 kupitia kwa Khamis Mcha kwa shuti akitumia vema pasi ya kichwa ya Shaban.
Wakati Azam wakidhani kuwa wamemaliza kazi, Shaaban Kisiga akaisawazishia Ruvu Shooting bao dakika za mwishoni na kufanya matokeo hadi mwisho wa mchezo kuwa sare ya 2-2 na timu zote kugawana point.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha point 11 katika michezo 7 iliyocheza ikiwa nafasi ya 4 nyuma ya Yanga yenye point 12.

Post a Comment