0

Mkutano mkuu wa wananchi wa vijiji vya Namayana na Elkurei wilaya ya Arumeru kujadili changamoto zao umeingia dosari baada ya uongozi wa mji mdogo wa Ngaramtoni kutangaza kuwa ofisi za serikali za vijiji hivyo zinatakiwa kuondoka kwenye jengo walilomo kwakuwa ni jengo la chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Arumeru hali iliyozua vurugu na malumbano makali kati ya viongozi na wananchi.

Hali hiyo imetokea katika mkutano wa wananchi baada ya mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Ngaratoni Sophia Soko na diwani wa kata ya Kiranyi kutangaza kuwa wenyeviti na watendaji wa vijiji hivyo wanatakiwa kuondoka kwenye jengo hilo kwa madai kuwa ni jengo la CCM ndipo hali ikachafuka ghafla.

Baadae wananchi wakaeleza msimamo wao kuhusu agozi hilo wakidai kwa zaidi ya miaka ishirini ofisi zimo kwenye majengo hayo na hawajawai kusikia kauli hiyo.

Post a Comment

 
Top