0

Waziri ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi  ameshangwazwa na baadhi ya wananchi kutafsili serikali ya awamu ya tano inawanyanganya wawekezaji wenye mashamba makubwa na kudai kuwa bado inawaitaji wawekezaji hao katika kutekereza azma ya serikali ya viwanda huku akiwataka kufuata taratibu na sheria.

Akiongea na wakati wa akisikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Kilombero waziri Lukuvi amesema matatizo ya migogoro ya ardhi yamekua ikipelekwa kisiasa wakati inatakiwa kufuata sheria huku akiwataka wananchi kuacha  kutafsili serikali ya awamu ya tano inania ya kuwanyanganya wenye mashamba makubwa kutokana na hivi karibuni kunyanganya baadhi ya watu wenye  mashamba kwa kushindwa kuyaendeleza.

Akitatua na kuskiliza zaidi ya migogoro 100 iliwasilishwa na wananchi wa kilombero lukuvi amesema bado serikali inaeshimu mhimili wa mahakama katika maamuzi yake ikiwemo mgogoro wa mashamba yanayo milikiwa na taasisi ya St. Marrys.

Post a Comment

 
Top