Kinondoni yajikita kutatua ajira kwa vijana.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jijini Dar es Salaam leo septemba 21 mwka 2016.
WILAYA ya Kinondoni imezindua kampeni ya wajasiriamali kwa vijana ili kuweza kutatua changamoto ajira kwa vijana na wananchi wa Wilaya hiyo.
Akizungumza na watendaji wa Wilaya hiyo wakati wa uzinduzi kampeni ya ujasiriamali, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa wananchi wakipata mafunzo ya ujasirimali itasaidia fursa kuongeza ajira kwa vijana.
Amesema mapato mengi yanayokusanywa kwa wilaya ya Kinondoni yanatokana na watu walioweza kujiajiri wenyewe wakaweza kuajiri watu wengine.
Hapi amesema kuwa vijana wakipata mafunzo ya ujasirimali kutasaidia kuondokana na kujiingiza katika vitu visivyo ikiwemo maandamano yasiyokuwa na tija , kujiingiza katika makundi ya uhalifu pamoja uzurulaji.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yataanza kwa walimu 30 ambao wakimaliza mafunzo hao watafundisha vijana wengine katika maeneo mbalimbali ujasiriamali wa kilimo cha mbogamboga, mama lishe ,ufugaji.

Post a Comment