0
 Ghala kuu la chama cha ushirika cha msingi umoja (UMOJA AMCOS) liliopo wilaya ya Liwale mkoani Lindi linauwezo wa kuhifadhi korosho tani 5,000-10,000 kwa pamoja na kipindi cha ununuzi wa mazao hutoa ajira za muda mbalimbali,akina mama rishe na kwenye nyumba za wageni muda huo hunufaika pia kwakuwa kuna ongezo la watu na mzunguko wa pesa unawepo.

 Ujenzi waanza wa kuweka mizani kubwa ya kisasa  itakayopima uzito wa magari katika ghala kuu la mnada la chama cha ushirika msingi umoja (UMOJA AMCOS) mizani hiyo itakuwa na uwezo wa kupima uzito wa tani 80 kwa pamoja lengo likiwa kurahisisha zoezi zima la shughuli za upokeaji wa korosho na kuhifadhiwa ghalani hapo na wakati wa ununuzi kwa njia ya mnada.

Kukamilika kwa ufungaji wa mizani katika ghala hilo itawavutia zaidi wanunuzi wa koshoro na kuongeza ajira za muda kwa wakazi wa Liwale  wakati wa zoezi la mnada watika eneo hilo
 Kuweka kwa mizani hii katika ghala kuu hili la mnada hapa wilayani Liwale itarahisisha kazi na itawavutia wanunuzi wengi kuja kununua korosho na kupunguza baadhi ya ghalama.
 Katika zoezi hili la kujenzi wa eneo la uwekaji wa mizani ya kisasa baadhi ya wakazi wa Liwale wameweza kupata ajira ya muda

Post a Comment

 
Top