Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA
leo Septemba 21 2016 limetangaza mabadiliko maalum ya michuano ya kombe
la mataifa ya Ulaya (EURO2020) litakalofanyika mwaka 2020, UEFA wametangaza mabadiliko ya sehemu ya michuano hiyo itakayofanyika.
Tofauti na miaka ya nyuma michuano hiyo
huwa inachezwa katika taifa moja ambalo huchaguliwa mapema na kuwa
mwenyeji, safari hii michuano ya Euro 2020 itafanyika katika miji 13 barani Ulaya, lengo likiwa ni kusherehekea miaka 60 ya michuano hiyo.
Mwaka 2020 michuano ya Euro itakuwa
inatimiza miaka 60 toka kuanzishwa kwake mwaka 1960, ni miji 13 ya nchi
13 barani Ulaya ambayo itakuwa mwenyeji, miji iliyotajwa ni Munich, Baku, Rome, St Petersburg, Brussels, Copenhagen, Budapest, Amsterdam, Dublin, Bucharest, Glasgow, Bilbao na London. CLICK >>>HERE
Post a Comment