Mchezqaji wa Sido fc akimilikli mpira (mwenye jezi nyukundu) kwenye mchezo wa jana waliocheza na timu ya Kigwema fc
Ligi ya Alizeti Cup Septemba mosi 2016 hatua ya robo fainaili iliendelea
kutimua vumbi kama kawaida kwa mchezo mmoja michuano hiyo timu ya Sido fc dhidi ya Kigwema fc katika
uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Timu ya Sido fc imeweza kuendeleza kutoa kichapa kingine kwa timu ya Kigwema fc mabao 6 kwa 2
katika ushindo huo mnono wa Sido fc Kibiga Kibiga aliweza kutisa nyavu mara 5 peke yake.
Katika kipindi cha kwanza Sido fc iliongoza kwa magoli 2 yalifungwa na Kibiga Kibiga namo dakika ya 4 na Kibiga Kibiga dakika ya 21 magoli yaliodumu mpaka 45 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili dakika ya 51 Abuu Kazumari aliiandikia Sido fc goli na Kibiga Kibiga aliendelea kutikisa nyavu tena mara 3 katika dakika ya 64,79 na dakika ya 89.
Magoli ya Kigwema fc yalifungwa na Abibu Ngongoya dakika ya 62 ambaye aliingia baada ya dakika 60 na akaiandikia timu yake goli la kwanza na goli la pili la Kigwema lilifungwa na Mikidadi Mola dakika ya 69 kwa mkwaju wa penaiti.
Kocha wa timu ya Kigwema fc,Meshaki Mpenga akizungumza na
Liwale Blog alisema matokeo ameridhika nayo kwani kushiriki kwao imekuwa faraja kubwa licha matokea aliongeza kusema kupoteza kwa mchezo huo kutoka na hali ya uwanja si mzuri sana pia alipongeza kamati ya mashindano kuweza kuwashirikisha nao kuweza kushiriki na wanajipanga upya wa mashindano yajayo.
Nae kocha wa Hawili fc,Mohamedi Hema alisema ushindi ni kawaida yao na inaisubili timu ijayo kuipa kichapo na ameomba fainali kukutana na timu ya Hawili fc japo kutakuwa na mchezo mgumu lakini atahakikisha anachukua kombe kwa mara ya pili.
Matokeo ya mchezo wa Agosti 31 kati ya timu ya New Boys
dhidi ya Super star mpaka kipindi cha pili 90 ilikuwa sare ya goli 1 kwa 1,goli la timu ya Super star lilifungwa na Hamisi Mkungura dakika ya pili huku goli la kusawazisha la New Boys likifungwa na Salumu Mpelembe katika dakika ya 49.
Baada ya dakika 90 ikafikia hatua ya mikwaju ya penaiti katika hatua hiyo New Boys iliweza kutikisa nyavu mara 4 na Super star ikitikisa nyavu mara 2,kwa matokeo hayo New Boys iliibuka na ushindi wa magoli 5 kwa 3 na kuweza kusonga mbele.
Leo septemba 2 kutakuwa na mchezo tena wa hatua ya robo fainali kati ya timu ya Mihumo City dhidi ya Kitogoro fc mchezo utakaopigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.
Post a Comment