SEHEMU
YA MWISHO
Aliongea kwa upole sana mwalimu kuliko hata
kawaida yake, huku akinisihi niwe mvumilivu katika kipindi kama kile, maongezi
ambayo kaisi kikubwa yalikuwa yanamuongelea mama yangu, kutokana na simu
aliyopokea kutoka kwa mjomba wangu. Ni hiyo simu iliyokuwa ikieleza hali ya
mama baada ya kufanyiwa mambo ambayo kiukweli yalionekana dhahiri upande wangu hayakuwa
madogo hata kidogo na mke wa mjomba, ajabu sasa sikujua chanzo cha yale yote,
nikakumbuka vyema kabla sijaondoka nyumba katika miezi miwili na nusu iliyokuwa
imepita kulikuwa na hakuna maelewano mazuri kati ya shangazi na mjomba, huku
mjomba akidai kukimbiwa na mwanamke huyo, kimbilio kubwa likiwa kwa mama.
Moja kwa moja nilijiua wazi uwenda katika
matatizo yale ya mjomba na mke wake, itakuwa ndio chanzo cha mama kuingia
katika matatizo. Nililani vikali mwanamke yule huku nikijenga gadhabu kali
ambayo muda ilikuwa imepotea dhidi ya viumbe viitwavyo wanawake, nikijiapiza
kufanya kitu juu ya kile.
Kiukweli hata sikuweza kuendelea kumsimkiliza
tena mwalimu licha ya kuniambia mjomba alitoa tu taarifa zile si kwajili ya
mimi kwenda nyumbani bali nikunijulisha jinsi mambo yalivyo. Nadhani alikuwa
amekosea sana maana akili yangu ilikuwa mbali sana. Nilijiuliza maswali mengi
ambayo majibu yake yalikuwa mbali, kwa wakati ule.
Huku mwalimu Rajabu akiendelea kunisihi sana
nisiweze kuwaza jambo lile, uwenda mambo yatakuwa sawa muda si mrefu. Lakini
maneno yake nilivyokuwa nikiyapiama kwenye mizani ya kichwa changu, yalionekana
dhahiri mama anaweza kuwa katika hali ambayo haikuwa si nzuri hata kidogo.
Kingine kibaya ambacho kilinitia shaka, mwalimu Rajabu alionekana kama kuna
jambo ananificha katika maongezi yake.
Nilimwitia mwalimu katika namna ambayo
ilikuwa ni kama kumlidhisha kwa muda
ule. Huku akili yangu ikiwaza kutoroka shule ilikuweza kwenda nyumbani mapema
iliniweza kujua hali ya mama. Kutoka na shule haikuwa mbali sana na nyumbani
yaani ilikuwa katika ndani ya mkoa ya Dar es salaam, ambapo nyumbani kwetu ilikuwa
Chanika yenyewe ikiwa kigamboni. Haikunipa
shida sana katika zoezi la kutaka kuondoka ndani ya shule. Japo kuwa sikuwahi
kutoroka hata siku moja lakini njia zote ambazo wazoefu wakutoroka shule
nilikuwa nazijua vilivyo.
Baada ya kutoka ndani ya ofisi ile, huku
akili yangu ikiwaza kufanya jambo lile hakunichukua muda sana, nilimuendea
rafiki yangu moja na kumwambia suala lile ambalo lilikuwa linanikabili na uzuri
mara nyingi huwa ananisikiliza sana. Hata nilivyomwambia jambo lile hakuleta
kipingamizi. Huku akinisihi niweze kurudi shuleni mapema sana kutokana na
mtihani ambao ulikuwa unanikabili katika majuma kadhaa ya mbele.
Alinisadia sana, ndugu yule katika
kukamilisha zoezi langu la kutoroka, japo nilikuwa na ujasiri hakika kidogo
ilijenga hofu kwenye mwili wangu, hofu iliyoletwa na kukumbuka habari za wahuni
ambao huwa mara nyingi wanakaa nje kwajili ya kuvizia wanafunzi ambao mara
kadhaa hutoroka, katika mpango ambao mwalimu mkuu aliweka katika kuthibiti
utorokaji wanafunzi shuleni pale. Ambao watu hao wakifanikiwa kukamata
wanafunzi wanawaleta shule na kupewa elfu hamsini kwa kila mwanafunzi
moja.
Hakika ilinipa hofu katika kufanya zoezi
langu lile, lakini nilipomkumbuka mama yangu ujasili ulinipanda, huku liwalo na
liwe likinitwala kichwani mwangu.
Uzuri mungu alikuwa upande wangu japo kuwa
hapakuwa na giza, kutokana siku hiyo ilikuwa mchana ambayo ilikuwa ikienda
jioni hivyo hata haikuweza kunisaidia kwa wale ambao walikuwa wakilinda
wanafunzi. Mungu tu ndio alifanikisha
lile mpaka na ingia kwenye gari la kuelekea Kongowe ambalo linginefikisha
kwenye gari Mbagala hapo ningepata gari za Gongo la mboto kisha kupanda gari za
nyumbani Chanika, hakuna kitu kibaya chochote ambacho kiliweza kunitokea,
nilishukuru Mungu sana kwa mara nyingine.
Safari haikuwa ndogo kabisa ndani ya siku
hiyo, kutoka na kubadilisha magari, huku foleni za hapa na pale zikiikabili
safari yangu. Ila hatimaye nilingia nyumbani huku sasa yangu ya mkononi
ikionesha vyema saa tano juu ya alama, ndio pua yangu ilikuwa ikininusa hali ya
hewa ya pale nyumbani.
Huku nikipokelewa na giza na ukimya ulikuwa
ukionesha dhahiri yakuwa mama hakuwepo pale, hilo nalo liliongeza hofu ndani
yangu, nikiangalia muda ulikuwa umeenda sana wazo la kwenda kwa mjomba kwa muda
ule lilikatishwa. Na juu ya kupata usafiri wa kunitoa pale na kunipeleka
nyumbani kwa mjomba, ambapo kulikuwa mbele ya Chanika, maana mjomba yeye
alikuwa akikaa Masaki ambayo ni mbele ya Chanika.
Akili yote haikuwa kabisa, niliendelea
kumlani shangazi kwa jambo ambalo wazi lilikuwa likionekana ni kubwa kufikia
mama kuhitaji uangalizi ambao mpaka muda ule sikuwa na jua ya kwamba ni
hospitali au nyumbani kwa mjomba.
Hakika mungu alikuwa upande wangu katika
jambo lile japo nilikuwa nimechanganyikwa sana kutokea shuleni lakini sikuweza
kusahau funguo za nyumbani, ambazo nilikuwa na miliki, maana mama
alishanizoesha kuniachia funguo, huku yeye akibaki na funguo zingine. Nilitafakari kidogo nikajitoma ndani baada ya
kutoa mahali funguo nilipoziweka.
Kweli baada ya kufanya zoezi la kufungua
mlango, nilikaribisha ndani huku nikiziendea taa ilikuweza kunipa mwanga ndani
mule, taa nazo hazikuwa na hiyana zilikubali nami na kuanza kunikaribisha.
Katika namna ambayo sikuitegemea. Nyumba ilikuwa imebadilika sana, kulionekana
dhahiri uwenda kulitokea purukushani ambayo haikuwa ya muda mrefu sana maana
vitu havikuwa katika mpangilio wake kabisa.
Hali ile nayo ikadhidi kuleta dhahama kwenye
kichwa changu, huku nikijenga taswira ya jambo ambalo lilikuwa kama giza ndani
ya fikra, hakika fikra zilionekana kunisaliti maana hazikuniletea jibu sahihi
kwa nyakati kama zile, si hivyo tu hata usiku nao ulikuwa mrefu sana kwa upande
wangu.
Uchungu ulikuwa umenikamata vilivyo, huku
taswira ya mama ikininyanyasa ndani ya usiku ule, na kiri wazi upendo nilikuwa
nao dhidi ya mama yangu haukuwa na kipimo ndugu msikilizaji.
Hatimaye asabuhi, ambayo ilikuwa kama mwaka
ndani ya usiku. Iliingia katika namna ambayo hakunihitaji hata kuoga zaidi ya
kubadili nguo, na kuongoza njia ya kuelekea kituoni, kuangalia gari ambazo
zingeniwezesha kufika kwa mjomba. Sikupata tabu sana, baada ya dakika kadhaa
nilikuwa ndani ya gari, ambayo hatukutumia muda mwingi hatimaye nilifika,
nyumbani kwa mjomba. Huku nikaribishwa
na ukimya ambao, nao ulizidi kunijengea hofu kwenye kichwa changu, kiukweli
nilishanganyikwa maana, hata miguu yangu haikuweza kusimama nikiwa pale.
Nilinyongonyea, kabisa sikuwa na nguvu ndugu
msikilizaji, hata muda ulivyokuwa unaenda nikiwa nje ya nyumba ya mjomba
sikujua, nilishangaa tu jua likiniwakia nikiwa pale lakini halikuwa na tija
kabisa kwenye mwili wangu.
Wakati nikiwa kwenye tafakari nzito, ni
nyakati hizo ambao kidogo nilipokea tumaini ambalo lilikuwa lishapotea kwa
upande wangu, hakika nilifulizia maswali mia kidogo mjomba ambaye alikuwa mbele
yangu, maswali ambayo sikumbuki kama mjomba alinijibu au la. Nilichokumbuka tu
mjomba alinisihi nitulie kwa muda ule, na ikiwezekana niweze kurudi shule mara
moja, jambo ambalo kwa upande wangu halikuwepo kabisa. Kuhusu kurejea shuleni
huku sielewi hali ya mama hilo lilikuwa jambo ambalo hakika nisingiweza
kulifanya hata ingekuwa kwa kupigwa ama.
Baada ya mjomba kuona nilikuwa nikileta
ukinzani kwa kile alichokuwa anaongea, alinisihi ni msikilize kwanza, nami
sikubisha nilimpa nafasi ya kujieleza, maneno ambayo kamwe yalizidi kuongeza
hasira kwangu na kuapa kufanya jambo baya dhidi ya shangazi, ambalo sikuwahi
kufikiria uwenda lingiweza kutimia katika namna ambayo ingenigharimu kwa kiasi
kikubwa.
Ukweli tulifika hospitali baada ya mvutano
dhidi yangu na mjomba kuangalia hali ya
mama ambaye, niilibaini haikuwa nzuri kwa wakati ule kutokana na shambulio la
aina yake alilofanya shangazi, la kujeruhi vibaya upande wa kushoto wa kifua .
Kutokana na dai lake la kuwa ndio chanzo cha ndoa yake kuvunjika dhidi ya
mjomba wangu. Niliumia sana kutokana na jambo lile huku nikijiapiza kufanya
kitu, kwa vyovyote vile ningefanya.
Najua chuki nilizokuwa nazo dhidi ya viumbe
viitwavyo wanawake, ndio ilikuwa chanzo ya kufanya yale yote, hata kama
shangazi alikuwa amefanya kosa lakini sikupaswa kuhukumu kwa namna ile. Wakati
mama yangu aliweza kupona mapema ila mimi nilijichukulia mamlaka ya kufanya
hukumu. Ukweli kabisa nilihusika katika kifo cha shangazi lakini sikusudia
kufanya mauaji.
_______
Lakini sikuwahi kufikiria uwenda kwenye jambo
langu lile zito ningesaidiwa na kiumbe ambaye katika maisha yangu niliwatoa
thamani viumbe vyote vya jamii yake. Naichukia nafsi yangu sana, chuki
zisiokuwa na msingi ndio ilikuwa chanzo yote yale, naweza sema maumivu ya moyo
ya kaka yangu kipenzi Eddy ndio yalinifanya nifike kule.
Hakika nimejifunza kitu kwenye kesi yangu
ile. Mwanamke aitwaye Catty ndio alikuwa amenisaidia sana katika jambo lile.
Sasa niliamua kuliweka wazi kila moja
aweze kuelewa kitu ambacho kilikuwa kipo nyuma ya jambo lile. Wanafunzi wenzangu,
mama yangu, mjomba yangu waweze kuelewa nini chanzo cha yale yote katika
nyakati zile.
________
Yalikuwa maneno yangu ya mwisho juu ya mambo
yalikuwa yamenitokea miaka kadhaa ya nyuma, maneno ambayo katika siku ile
nilipokuwa nikiyatoa yalimtoa mama yangu chozi sana. Hakika mama yangu alitambua
kiasi gani moyo wangu ulivyokuwa ukimthamini kaka yangu pamoja nae. Najua
aliteseka sana, katika muda wote nilivyokuwa ndani katika kesi iliyokuwa
ikinikabili ya kuuwa, lakini baada ya msaada mzuri wa mwanasheria Catty,
niliweza kuachiwa huru kwa kosa lile huku likihesabika kama ni kosa la kuua
bila kukusudia. Yale yote yalinifanya nijifunze jambo katika maisha yangu yote
nanyi ningependa mjifunze kupitia mimi.
Mwisho
Hakika ilikuwa tetemeko la moyo, naimani umejifunza kitu kwenye
kazi. Hii pia ningependa kushukuru katika kuifatiria kazi hii, kuanzia mwanzo
hadi mwisho. Ningeomba tena uendelee kufatiria kazi zingine za mwandishi mahiri
Yona fundi. Kwa maoni na ushauri
wasiliana nasi kupitia namba zifatazo 0675278759.
SIMULIZI
MARIDHAWA. TETEMEKO LA MOYO
NA MWANDISHI. YONA FUNDI.
MAWASILINO :0675278759.
NA MWANDISHI. YONA FUNDI.
MAWASILINO :0675278759.
NA KURUSHWA NA LIWALE BLOG,INAKUJA SIMULINZI NYINGINE MPYA NA KALI ZAIDI.
Post a Comment