0

 Mchezaji wa timu ya Kitogoro fc (mwenye jezi ya blue) akimiliki mpira kwenye mchezo wa leo wa kumtafuta mshindi wa tatu ligi ya Alizeti cup
Timu ya Kitogoro fc leo septemba 8 imeweza kuchukua nafasi ya tatu baada ya kuichapa timu ya New Boys magoli 4-1 mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza namo sekunde ya 30 Kitogoro fc ilitikisa nyavu goli lililofungwa na Hamza Gochigochi na goli la pili la Kitogoro fc ilifungwa na Jastino Monga dakika ya 44 huku goli la New Boys likifungwa na Jafari Mpelembe dakika ya 43.

Katika kipindi cha pili Kitogoro fc iliongeza magoli 2 yaliofungwa na Abasi Mbukuli dakika ya 69 na Rama Malibiche dakika ya 85 mpaka mchezo mwamuzi anapuliza kipenga Kitogoro fc iliweza kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 na kuweza kushika nafasi ya 3.

Kesho septemba 9 kutakuwa na mchezo wa Fainali kati ya timu ya Hawili fc Vs Sido fc mchezo utakaopigwa uwanja wa wilaya majira ya saa 10 jioni na unatarajiwa kuwa na watazamaji wengi zaidi.
 

Post a Comment

 
Top