Ibada ya Hajj
nchini Saudia imefika kilele chake huku takriban Waislamu milioni 1.5
wakikongamana katika mlima Arafat ili kufanya maombi ya siku nzima
mbali na kusoma Quran.
Mahujaji hao walikongamana katika mlima huo wakati wa macheo ambao uko takriban kilomita 15 kutoka mji wa Mecca. Mahujaji wakongamana katika mlima Arafat
Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho katika eneo hilo.
Nguzo ya Hajj ni mojawapo ya nguzo tano za kiislamu ambayo Waislamu hutakiwa kuitekeleza ijapokuwa mara moja. Mahujaji wakongamana katika mlima Arafat huku baadhi yao wakisoma Quran
Siku ya Jumamosi ilibainika kuwa kiongozi mkuu wa
dini nchini Saudia Abdul Aziz al-Sheikh hakuweza kutoa hotuba yake ya
kawaida kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35 kutokana na
matatizo ya kiafya.
Post a Comment