0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Temeke kimemvua uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Matiti Togocho kwa tuhuma za ufisadi dhidi ya wananchi wa kata hiyo.
Makamu Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke Bernard Mwakyembe amesema kuwa Tochogo mnamo Novemba 23, 2015 na wenzie walitengeneza hati feki za nyumba tano za James Makundi na kulidanganya Jeshi la Polisi kuwa Makundi alikuwa mpangaji ambapo alifanikiwa kufanya hujuma na kuvunja nyumba hizo kwa oda ya uongo iliyotolewa na Wakili Samora Avenue badala ya oda halali ya mahakama kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa mwekezaji zaidi ya milioni 250.

Pia amesema diwani huyo alishiriki kudhurumu pesa kiasi cha sh milioni 138 kwa kushirikiana na msimamizi wa mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni huku akijua kuwa kesi iko mahakamani, pamoja na kuvunja nyumba tatu za marehemu huyo na kuiacha familia yake kukosa makazi.

“Utapeli mwingine alioufanya ni kudhurumu kiasi cha sh. 42,000,000 ambayo ilikuwa fidia ya Paulina Shabani na wajukuu zake. Pia Mwaka 2015 aliidhinisha kutoa eneo la wazi kwa mwemezaji Kilimanjaro Cables (T) Ltd bila kishirikisha wajumbe wa seriakali ya mtaa na badala yake alitumia wajumbe feki kwa lengo la kujipatia fedha, ” amesema Mwakyembe.

Amedai kuwa mnamo Juni 26,2016 Tochogo alihujumu uchaguzi wa ndani ya chama katika kata ya Kurasini kwa kuita polisi ili wazuie uchaguzi huo kwa lengo la kusababisha chama hicho kukosa uongozi ili kuendelea kufanya ufisadi.

“Tukiwa kama chama ngazi ya wilaya ambao tunawajibu wa kusimamia masilahi ya chama ngazi husika leo tumefikia maamuzi ya kumfukuza uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini Matiti Togocho baada ya kujiridhisha na makosa yote ya ufisadi aliyowafanyia wananchi wa kata hiyo, ” amesema.

Ameongeza kuwa “Kutokana na Maamuzi ya chama baada ya kujiridhisha na makosa yake na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu mamlaka ya mwisho ya kumwondoa nafasi yake ya uongozi ni wilaya na nafasi ya udiwani wenye maamuzi ya kumuondoa ni kamati kuu ya chama.”

Aidha, Mwakyembe amesema kabla ya kufikiwa maamuzi hayo ya kumfuta uanachama Tochogo, kamati ya chama hicho ngazi ya wilaya kilimuita mara kadhaa kufanya mazungumzo lakini haluitika wito, na kwamba siku alioitikia wito ambayo ilikuwa jana wakati wa mahojiano hakutoa uahirikiano na kutishia kuita jeshi la polisi.

“Tulimuita hakuitikia wito awali alipokuja akatuambia maneno ya kejeli kuwa vikao vya ndani vimeaghirishwa na kwamba ataliambia jeshi la polisi kuja kutukamata. Tochogo aelewe kuwa

Tupo kwa ajili ya kutumikia wananchi, na tutadili na madiwani wote wanaofanya mambo kinyume cha taratibu, ni bora tuwe nao wachache waaminifu na waadilifu kuliko kuwa na wengi ambao si waaminifu, ” amesema.

Na Regina Mkonde 

Post a Comment

 
Top