0



                              .
September 21,  2016 imetokea ajali ya barabarani jijini Mwanza ambayo imehusisha mabasi mawili likiwemo basi la Super Shem lenye namba za usajili T 874 CWE ambalo lilikuwa likitokea Mbeya limegongana na Basi dogo aina ya Hiace yenye namba za usajili T 368 CWQ iliyokuwa inatokea kijiji cha Shirima na kusababisha vifo vya watu 11 na majeruhi kadhaa.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi ambapo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali kuwa ni Hiace iliyogongwa na basi la Super Shem kuingia barabara kuu bila kufuata sheria. Ajali hiyo imetokea eneo la Mwamaya Makutano Kwimba.

>>>Kati ya waliofariki, wawili ni watoto wadogo, majeruhi saba huku miili ya marehemu na majeruhi wakikimbizwa Hospitali ya Ngudu, Dereva wa Super Shem alipata madhara, lakini wengi zaidi waliopata madhara ni kutoka kwenye Hiace ndiko kuna matatizo makubwa:- Kamanda Ahmed Msangi



Post a Comment

 
Top