BODI
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema haiwezi kutoa
mikopo kwa waombaji wapya walioomba baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
kushusha viwango vya udahili.
Wiki iliyopita, TCU ilitangaza kushusha viwango vya udahili bila kueleza sababu za kufanya hivyo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa,
amesema tume hiyo haiwezi kuongeza muda kwa wanafunzi wapya kwa ajili
ya kuomba mkopo kutokana na mchakato huo kufungwa.
Amesema
tofauti na tume ya vyuo vikuu ambayo inaweza kufungua udahili na kutoa
majina ya wale waliopata nafasi ndani ya siku tatu, HESLB huhitaji muda
mrefu kupitia taarifa za waombaji hadi kutoa matokeo.
Kuhusu
marejesho ya mikopo kwa wahitimu wa elimu ya juu waliokopeshwa na bodi
hiyo, Mwaisobwa amesema idadi kubwa ya wadaiwa na waajiri wamejitokeza
kulipa madeni yao na kuhakiki taarifa za madeni yao.
“Idadi
kubwa ya wadaiwa wamejitokeza kulipa na kuhakiki taarifa zao, pia hata
waajiri wengi wamejitokeza na kuthibitisha hili ni kwamba mapato
tuliyokusanya yameongezeka kwa kiasi kikubwa” amesema Mwaisobwa.
Amesema
wanaokaidi kulipa, watambue kuna sheria zitakazowabana, ikiwa ni pamoja
na vifungo na penati, lakini hilo halitangulizwi bali mpaka mkopaji
aonekane kukaidi.
Post a Comment