Rais John Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu) |
SERIKALI
imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi
kutoka Kabaale katika wilaya ya Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga,
nchini.
Uamuzi
huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana,
Ikulu, Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais John Magufuli.
Taarifa
ya hatua hiyo ya serikali kuridhia rasmi ujenzi wa mradi huo ilitolewa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao hicho.
Majaliwa alisema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa, unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola
za Marekani bilioni 3.5 na kati ya fedha hizo dola bilioni tatu
zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.
Mradi huo
mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikisha
kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na
Serikali mbili za Tanzania na Uganda.
Majaliwa
alisema kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa
kusafirisha mapipa ya mafuta ghafi 200,000 kwa siku na kila pipa
litaliingizia taifa dola za Marekani 12.2.
Post a Comment