Wanachama wa tume
ya Uchaguzi mkuu nchini Gabon wametangaza kuwa rais Ali Bongo,
amehifadhi kiti chake cha urais baada ya kumshinda mpinzani wake Jean
Ping.
Ushindi huo ni baada ya kumalizika kwa shughuli za upigaji kura, hapo siku ya Jumamosi.
Lakini
mwaandishi wa habari wa BBC mjini Libreville, amesema kuwa wajumbe
wanaowakilisha upinzani katika tume ya uchaguzi, wameondoka ndani ya
ukumbi wa kuhesabu na kusawazisha matokeo ya kura, na kukataa kutia
saini hati zinazompa ushindi rais Bongo.
Walinda usalama wanapiga doria katika barabara za mji mkuu Libreville huku taharuki ikitanda kote nchini humo.
Familia
ya Bongo imetawala Gabon kwa nusu karne huku Omar Bongo akitawala kwa
miongo minne, na mwanawe rais wa sasa Ali, alichukua hatamu za uongozi
mnamo mwaka wa 2009.
Post a Comment