0

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetoa onyo kwa yeyote atakayejaribu  kudhoofisha  ama  kukwamisha  jitihada  za  kulinda  hifadhi  za  taifa ,mapori  ya  akiba  na  misitu huku ikitaka suala la mifugo kuingizwa katika hifadhi za taifa lisichukiliwe kisiasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema  hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Mlele mkoani Katavi.

Amesema kwa watakao bainika kudhorotesha jitihada hizo watashughulikiwa  kikamilifu  kwa  mujibu   wa  sheria  na  kwamba   agizo   la  serikali   la  kuhakikisha  rasilimali  hizo   zinalindwa  kwa  faida  ya  kizazi  cha  sasa  na  kijacho  linatekelezwa  kwa  vitendo .

Kwa upande wake Mkurugenzi  mkuu  wa  tanapa  Allan  Kijazi  anasema  jitihada  za kuimarisha  ulinzi  zimeanza  kuzaa  matunda katika hifadhi mbalimbali hapa nchini huku Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Fred Manongi amesema mabadiliko ya utendaji kazi wa taasisi zilizo chini wizara ya maliasili na utalii kwa kiasi kikubwa yameanza kupunguza matatizo  yaliyokuwa  yanatishia  uhifadhi   likiwemo  suala la la  ujangili.

Post a Comment

 
Top