0

 Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena na wafanyakazi wa Trumark Tanzania wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.

   Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba akizungumza na wanawake 150 katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililofanyika Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi wa Trumark, Agnes Mgongo akitoa somo la fursa kwa wanawake wapatao 150 waliohudhulia katika ufunguzi wa jukwaa la wanawake kuwezeshwa kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MIBOSCO, Moses Emena akizungumza na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

WANAWAKE wapata mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi pia wamehimizwa kutambua fursa za kiuchumi, kupambana na changamoto mbalimbali zinazomzunguka pamoja na kujihusisha katika shuguli za vikundi ili  kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.

Hayo yamabainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena  wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi  lililofanyika leo kunduchi Mtongani jijini Dar es salaam leo.

Jukwaa hilo limewakutanisha Wanawake wapatao 150 likiwa na lengo la kuwapa elimu wezeshi Wanawake katika  harakati za  kutokomeza umaskini na kupambana na unyanyasaji wa aina zote ndani ya jamii zetu kwa kuendeleza elimu, haki na uhifadhi wa mazingira .

Moses Emena  amesema “ Jukwaa hili limedhamiria kuleta mwamko na hamasa chanya kwa Wanawake wa eneo hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi.” ameongeza kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo, katika harakati za kupamba na umaskini.

Emena  pia  amewashkuru wawezeshaji wa mafunzo hayo  Kampuni Trumark kwa kukubali kujitolea kutoa mwongozo wa maandalizi na kutoa elimu wezeshi kwa Wanawake na kushirikiana nasi bega kwa bega katika kufanikisha siku ya leo.

Vile vile aliwashuru kwa dhati wadhamini na wadau wa maendeleo ya Wanawake Kampuni ya Vodacom Tanzania na Shirika la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kujitoa kwao kuwezesha,  bila kuwasahau wangeni waalikwa kutoka taasisi za fedha Akiba Commercial Bank, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, waandishi wa habari na wengine wote.

Post a Comment

 
Top