0


WANACHAMA wa Simba walitumia dakika 13 kuimba wimbo wa Mo..mo..mo..
kuhitaji mbadiliko ndani ya klabu hiyo katika Mkutano Mkuu uliofanyika
jana katikaa Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo, mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’, alitawala
kiasi cha wanachama hao, kutotilia nguvu ajenda zilizopita.

Wanachama hao walionekana kuwa wana hamu ya kuusikia uongozi wao
unasema nini kuhusiana na kuingia kwenye kampuni ambako Simba itaweza
kuuza hisa.

Uamuzi huo, ulisababisha wanachama kutotaka kujadili chochote zaidi ya
kuona kama uongozi uko tayari kuuza hisa zake asilimia 51 kwa Sh
bilioni 20 kwa Mo.

Wakati wa kujadili ajenda nyingine za kikao kama zile za Hesabu,
Kuthibitisha taarifa ya chombo cha ukaguzi na hatua zitakazochukuliwa
na vyombo vya utendaji na nyinginezo, hazikuwa na mvuto na wengi
walitaka ajenda namba tisa ambayo ilikuwa ni ‘Taarifa ya kamati ya
maboresho ya mfumo wa uendeshaji’.

Katika kutambulisha ajenda hiyo namba tisa, Rais wa Simba, Evans Aveva
alionekana kama kutohitaji ubadilishwaji wa mfumo huo baada ya kutoa
faida na hasara zake.
Lakini wanachama hao walianza kulalamika wakiona kama uongozi ulipita
haraka hapo, ndipo wakaanza kupiga kelele wakitaka kusikia mjadala
ukipewa uzito.

Wanachama hao, walipiga kelele kutokana na kauli tata ya Aveva kuanzia
saa 6:47 hadi saa 7:00 mchana kwa kuimba wimbo wa
Mo….Mo….Mo……Mo…..Mo….! madiliko…. Madiliko…mabadiliko….!.

Mwisho, Rais wa Simba Evans Avena alilazimika kurejea na kuwaeleza
kwamba kama wanataka Simba kuingia kwenye mchakato wa kampuni, maoni
yao yamesikilizwa na yanaanza kufanyiwa kazi kwa kuigaza Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo kukutana na Mo ili kujadili uekezaji huo.

“Nimekusilizeni na maoni yenu nimeyakubali hivyo basi Kamati ya
Utendaji itakutana na Mo ili kujadili uwekezaji huu.

“Sisi tunakubali kama maoni yenu lakini Mo hajaleta barua yoyote
kwenye uongozi na taarifa zake tulikuwa tunazisikia kupitia vyombo vya
habari tu,” alisema.

Kauli hiyo ya Aveva, ilifanya wanachama hao washangilie kwa nguvu hata
yeye baada ya kuufunga mkutano huo na kumsindikiza hadi kwenye gari
yake.

Wanachama wavalia jezi za Mo

Wanachama wa Simba walionekana kuhitaji mabadiliko ndani ya klabu hiyo
kutokana na uongozi kufeli katika miaka mitatu mfululizo bila kuchukua
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hivyo basi, wanachamaa walionekana kuvalia jezi zenye picha Mo
iliyokuwa imepigwa ‘tiki’ pamoja na Said Salim Awadh Bakhresa ambayo
ilikuwa imepigwa ‘X’ kama ishara ya kushinikiza timu apewe
mfanyabiashara huyo.

Kutumia sh. Bil 4.4 msimu ujao
Klabu hiyo imepanga kutumia bajeti ya sh.4, 411, 025,000 katika msimu
ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao unatarajia kuanza Agosti 20,
mwaka huu.

Bajeti hiyo itatumia kwa gharama za uendeshaji wa klabu, za kifedha,
miradi ya maendeleo na madeni mbalimbali ambayo timu hiyo inadaiwa.

Wazee Simba watoa masharti mazito

Wazee wa klabu ya Simba walionekana kuingia hofu kuhusu uwekezaji huo
kutokana na kutokuwa na imani na Mo ambaye alikuwa anatoa ahadi hewa
toka zamani.

Wakongwe hao ndani ya klabu hiyo walifikia kutoa masharti mazito kwa
Mo kama kweli anahitaji kufanya uwekezaji ambao utakuwa na tija ya
kupata maendeleo.

Wazee hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Hassani
Dalali walisema kwanza wanahitaji kupata elimu ya kutosha kabla ya
kupewa klabu.

“Si jambo baya hili, lakini tunahitaji uelewa wa kutosha faida na
hasara kuhusu mfumo huu wa hisa, kama mimi nina miaka mingi humu hivyo
siwezi kuwa sawa na aliyeingia mwaka jana,” alisema Dalali.

Kwa upande wa mzee, Hamisi Kilomori alisema kuwa mashaka yake isije
baadae akajimilikisha ikawa klabu ya kwake endapo tu kutokana na
kushindwa kufunga mikataba vizuri.

“Tutampatia timu sawa, ila tunataka kujua nafasi ya wanachama inakuwa
wapi? Maana isiwe baaadae ikawa ndiyo klabu ya kwake na wanachama
hawana sauti, sasa tunataka tukutane nae tujadili kama akishindwa
kufuata matakwa ya timu atatupatia timu yetu?,” alisema.

Wakati kwa upande wa Bi Hindu alikuwa anahofu ya kuizamisha klabu hiyo
kutokana na kushindwa kuziendesha timu zake kama African Lyon na
Singida United ya Singida.

“Huyu ni muongo tu, anataka mali zetu, mbona zamani Simba inalia njaa
hakujitokeza? Yaani huyu anataka kutafuta fedha kupitia Simba.

“Zamani aliwahi kutuambia atanunua uwanja wa Sigara pale TCC Club
Chang’ombe (sasa CDS Park) lakini alishindwa kufanya hivyo sasa sisi
tunamashaka naye na kama anataka kuhisaidia Simba basi asajili
wachezaji mwaka huu na tufanye vizuri kuliko kuongea tu maneno mengi,”
alisema Bi Hindu.

Mkutano huo ulianza saa 5:00 asubuhi baada ya akidi kutimia ya
waajumbe 650 ambapo ulifikia tamati saa 7:00 mchana.

Post a Comment

 
Top