Shirikisho la Mpira
Miguu Tanzania TFF limethibitisha kwa CECAFA kuwa timu ya taifa ya
wanawake ya Tanzania itashiriki michuano ya kwanza ya Kombe la Chalenji
kwa wanawake.
Michuano hiyo itaanza Septemba 11,mpaka Septemba 20, 2016 kwa kushirikisha nchi saba wanachama wa shirikisho hilo.
Tanzania
itaanza kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, kabla ya kucheza na Ethiopia
2016. Ethiopia zitacheza Septemba 14, wakati kundi A Zanzibar itakata
utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.
Michezo
mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza
Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda.
Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.
Mashindano
ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo
linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake
kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tanzania inatarajiwa
kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani
kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa
safari ya Uganda.
Post a Comment