0

Dar es Salaam. Serikali imetangaza kuitambua Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) chini ya Rais Chaurembo Palasa kuwa ndicho chombo pekee kinachoruhusiwa kusimamia mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Kutokana na kauli hiyo ya Serikali,  mashirikisho maarufu nchini, TPBO-Limited chini ya Rais Yasin ‘Ustadh’ Abdallah, PST chini  na  Emmanuel Mlundwa na TPBC Limited chini ya Onesmo Ngowi hayaruhusiwi kusimamia mchezo huo kutokana na kutokuwa na usajili unaotambuliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia msajili wa vyama na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Katibu wa BMT, Mohamed Kiganja amesema TPBC, ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia mchezo huo, imesajiliwa  na BMT  na hawakuona haja ya kuendelea na mchakato wa kuunda chombo kimoja kinachosimamia mchezo huo kutokana na wajumbe wake wengi kuwa viongozi wa mashirikisho ambayo hayajasajiliwa.

Post a Comment

 
Top